Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni moja ya topic zinazokera na ngumu kuongeleka. Hii ni kutokana na kwamba wanawake huona aibu na kuhisi ni hali mbaya kwa mtu mwingine kuifahamu.
Utunzaji wa Uke na Usafi
Kutunza uke na kulinda afya ya uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke. Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni kiashiria kwamba unaumwa na hauko sawa. Hali hii inaweza kuathiri heshima ya mwanamke na pia mahusiano na mwenza wake.
Harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida. Japo siyo kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.
Kama wewe muhanga wa tatizo hili basi tambua kwamba kuna njia za asili unaweza kuzitumia ikiwemo lishe na virutubisho na ukarudi katika hali ya kawaida. Kesi chache sana kama tatizo litazidi kuendelea basi itatakiwa uende hospitali ili upate uchunguzi.
Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo la samaki basi ujue kuna tatizo kubwa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni huwa inaambatana na dalili zingine kama kuwasha na kuchomachoma na kutokwa na majimaji.
Nini Kinasababisha Harufu Mbaya Ukeni
Ukuaji wa Bacteria (Bacteria vaginosis)
Sababu namba moja ya kupata harufu mbaya ukeni ni ukuaji wa bacteria. Bacteria Vaginosis ni ukuaji wa bacteria usio wa kawaida kwenye uke. Rejea maelezo ya pale juu kuhusu sababu ya kukua kwa bacteria wabaya kwenye uke ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa mazingira ya ukeni na kushuka kwa kinga.
Bacteria vaginosis inaweza kupelekea mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mengine ya ngono. Dalili mojawapo ya kwamba tayari una maambukizi ya bacteria ni kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu kali mfano wa harufu ya samaki wabichi
Trichomoniasis
Trichomoniasis ni moja ya ugonjwa wa ngono unaosababisha harufu kali ukeni. Ugonjwa huu husababishwa vimelea na huambatana na kutokwa na uchafu ukeni,kuwasha, na maumivu makali wakati wa kukojoa.
Trichomoniasis inaweza kuwaathiri wajawazito na kuleta hatari ya mimba kutoka. Kama utagundua una Trichomoniasis basi wewe na mwenza wako mnatakiwa kutibiwa. Hakikisha pia unatumia condom vizuri kila unapofanya ngono kama kinga dhidi ya magonjwa haya.
Mabadiliko ya Homoni
Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wapo kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana na hivo kusababisha tishu za kuwa na tindikali kidogo.
Kutozingatia Usafi na Kutokwa sana na Jasho
Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya. Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (apocrine sweat glands )hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo ya mwili.
Maeneo haya ni kama kwapa, pua, ndani ya sikio, uke, na kwenye chuchu. Bacteria waliopo maeneo hayo huchakata mafuta haya na hivo kuzalisha harufu kali. Uvaaji wa nguo zilizobana na uzito kupita kiasi huchangia kuhifadhiwa kwa jasho kwenye mikunjo ya ngozi na hivo kuletekeza harufu.
Kuvaa Pedi kwa Masaa Mengi
Pedi inapovaliwa kwa muda mrefu husababisha ngozi kucharuka,kututumka na kuwasha na pia. Hali hii huchangia kukua kwa bacteria na fangasi wabaya ambao ni chanzo cha harufu.
Hatua 6 za Kujikinga dhidi ya Harufu Mbaya Ukeni
1.Vaa nguo za ndani za pamba, zisizobana sana.
Nguo zilizoabana zinazuia kupita kwahewa safi kuelekea ukeni na hivo kusababisha unyevunyevu ambao ni mbolea kwa bacteria na fangasi wanaoleta harufu mbaya kwenye uke. Hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 inasaidia kuzuia kukua kwa bacteria wabaya.
2.Badili Nguzo zako Kila Baada ya Kufanya Mazoezi
Nguo zenye unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bacteria hivo hakikisha unavaa nguo zilizokauka na kubadilisha kila baada ya kutoka mazoezini.
3.Punguza uzito kama inawezekana
Uzito mkubwa na kitambi vinakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke. Na kama tulivojifunza pale juu, jasho na unyevunyevu inaleta fangasi na bacteria wabaya. Chagua kula lishe nzuri na kufanya mazoezi ili kurekebisha mwili wako. Unaweza kutuma kifurushi chetu cha weight loss package ili upunguze uzito wako vizuri pasipo kujinyima kula.
Epuka Kuflash Uke Kila Mara (Douching)
Kusafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali na sabuni inaharibu mazingira ya bacteria wazuri. Bakteria hwa ni walinzi, na hivo kuacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bacteria wabaya pamoja na fangasi wa candida.
Epuka Kutumia Spray na Marashi Ukeni
Ukweli ni kwamba ngozi ya uke ni laini sana kwa hiyo inanyonya kwa urahisi kemikali zilizopo kwenye spray kuingia kwenye damu. Usiingie kwenye mtego huu, kumbuka miili yetu imeumbwa kujisafisha yenyewe, Pale unapoongeza kitu cha ziada basi unaharibu normal flora na kuharibu kinga ya mwili.
Epuka Baadhi ya Vyakula Ambavyo ni Adui wa afya yako
Kuna aina nyingi ya vyakula ambavyo vianweza kukuathiri wewe kama mwanamke kwenye swala la uzazi. Vyakula hivi vinaharibu mazingira ya uke, kuua bacteria wazuri na kubadili PH. Vyakula vyenye sukari, Pombe, ngano na vyakula vilivyosindikwa huchochea ukuaji wa fangasi wa Candida.
Njia za Kutumia ili Kukata Harufu Mbaya Ukeni
Harufu kali kwenye uke mara nyingi inagundulika zaidi baada ya kufanya ngono na pia kwenye hedhi. Kwahiyo badala ya kukimbilia spray na kujisafisha ukeni ili kuondoa harufu tumia njia zifuatazo kwa muda kabla hujamuona dactari wako
Apple Cider Vinegar
Vinegar hii imejaa viini ambavyo ni antibacterial na antiseptic ambavyo vitakusaidia kupambana na harufu hii kali. Chukua kiasi kidogo cha vinegar changanya na maji kwa uwiano wa 1/10 na uoshe eneo la uke.
Baking soda
Baking soda inaweza kutumika ili kubalansi pH kwenye mwili. Kumbuka mwanzo tulivosoma kuhusu madhara ya kubadilika kwa pH. Ukibalansi pH basi tatizo la harufu kali linakuwa limeisha. Unaweza kutumia pia baking soda kama body spray na ukaepuka kujaza sumu mwilini.
Chukua kijiko kimoja cha baking soda weka kwenye ndoo na maji jagi moja, kisha osha uke kwa dakila 5. Jifute kwa taulo sehemu zote usiache unyevu kabla ya kuvaa nguo. Tumia mara mbili tu kwa wiki usizidishe.
Matunda na Mbogamboga
Matunda yenye uchachu mfano machungwa, mapera na strawberries yana Vitamn C kwa wingi sana ambayo ni huimarisha kinga ya mwili na kusaidia utoaji wa sumu mwilini. Chakula kama Parachichi na mboga za kijani ina Vitamn B6 na madini ya potasium ambayo huongeza hamu ya tendo la ndoa na kujenga kuta za uke hivo kuzuia hatari ya kushambuliwa mara kwa mara.
Kitunguu Saumu
Kitungu saumu kinafahamika tangua miaka ya zamani kwa uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kinga na kupambana na maambukii ya bacteria na fangasi. Unaweza kula kitunguu saumu kimoja kwa siku ama ukatumia virutubisho ambavyo vipo kwenye mfumo wa vidonge mfano Garlic oil softgel tunavyotumia kuwahudumia wagonjwa wetu
Karanga na Mbegu
Matumizi ya karanga na mbegu kwenye mlo wako wa kila siku huzuia kukauka kwa uke kwa sababu kuna Vitamin E kwa wingi. Unaweza kutafuna mbegu kama maboga, almond, karanga, walnuts na alizeti.
Maji safi ya Kunywa
Kiungo hichi cha uke chenye tishu laini kinahitaji maji ya kutosha ili kukiweka laini na hivo kupunguza harufu mbaya. Unapopata kiu usinywe soda kunywa maji ya kutosha.
Tembelea stoo yetu kwa kubonyeza hapa ili kuanza matumizi ya virutubishi vya asilia ambavyo vitakusaidia
- Kutibu chanzo cha tatizo lako la harufu mbaya ukeni (kutokana na vipimo vya tatizo)
- Kuimarisha kinga ya mwili na kuzuia maambukizi ya fangasi na bacteria
- Kuimarisha ukuaji wa bacteria wazuri na kurekebisha pH.
Muhimu kwa Wanawake wenye Muwasho na Hrufu mbaya ukeni
Kwa mwanamke mwenye changamoto ya muwasho na harufu mbaya ukeni, na hedhi kuvurugika, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na kutibu maambukizi. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama , harufu mbaya ukeni, muwasho, fangasi, PID na maambukizi ya bakteria
Vidonge hivi vinatumika kwa wiki moja. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24 ,unaweka tena kidonge kingine.
Gharama ni Tsh 50,000/=
Angalizo unapotumia Uterus Cleansing Pill
UCP haifai kutumiwa na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi na pia ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.