Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuungua kwa sehemu mbalimbali za tumbo kutokana na uwepo wa tindikali nyingi. Vidonda hivi vinaweza kutokea kwenye tumbo lenyewe, vinaweza pia kutokea sehemu ya mwanzoni mwa utumbo mwembamba ama vinaweza kutokea shemu ya juu kabla ya tumbo .
Dalili za Vidonda Vya Tumbo.
Vidonda vya kwenye tumbo lenyewe la chakula huwatokea watu wengi zaidi kulinganisha na aina zingine za vidonda tumbo. Vidonda hivi vinaweza kusababishwa na umwagaji wa tindikali nyingi kwenye tumbo, kutokana na mtu kuwa na msongo wa mawazo, lishe mbaya, uvutaji wa sigara, matumizi ya pombe, au uwepo wa bacteria wa h pylori. Karibu asilimia sabini ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo husababishwa na uwepo wa bakteria hawa hatari wa H pylori tumboni. Matumizi ya vidonge vya kupunguza maumivu kama ni moja ya vihatarishi pia kupata vidonda vya tumbo.
Hali ya kuungua tumboni ni dalili mojawapo kubwa sana ambayo kila mgonjwa wa vidonda vya tumbo huisikia. Maumivu haya ni kutokana na tindikali iliyopo tumboni inapogusa vidonda. Hapa chini ni dalili zingine za vidonda vya tumbo
- Maumivu kuwa makali zaidi pale unapokuwa hujala
- Kushituka sana usiku na kukosa usingizi
- Maumivu kupungua pale unapokula chakula
- Kupungua kwa uzito kwa haraka
- Kukosa hamu ya kula kutokana na maumivu
- Tumbo kujaa gesi na kujiskia umeshiba mda mwingi
- Kupata dalili za kuishiwa damu mfano, kuchoka sana, pumzi kukata.
- Kupata kinyesi cheusi kutokana na uwepo wa damu
Hakikisha unaonana na Daktari mapema iwezekanavyo unapoona dalili hizi. Hata kama ni za muda mfupi na kupotea, tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kadiri muda unavoenda mfano kupoteza damu kutokana na uwepo wa vidonda ni hatari kwa afya yako. Ni muhimu kufanya vipimo kupata uhakika na tatizo linalokusumbua kisha ufike ofsini nikwanzishie dawa ya chai.
Matibabu ya Vidonda Vya Tumbo
Matibabu ya vidonda vya tumbo hutegemea na chanzo cha tatizo. Kwa wagonjwa wengi hutibiwa kwa kuandikiwa dawa baada ya ushauri wa Daktari lakini kwa kesi chache sana huwa zinahitaji kufanyiwa upasuaji, hasa kama tatizo limekuwa kubwa zaidi. Ni muhimu kutibu vidonda vya tumbo haraka iwezekanavyo, endapo umepoteza damu nyingi sana basi utahitaji kuongezewa damu.
Tumia hii Tiba Asili kupitia mimea asili upone vidonda vya tumbo.
Majani ya chai ya in-cleasning pamoja na vidonge asili vya yashtmadhu vimekuwa vikitumika sana kwa Nchi za wenzetu na yameleta mafanikio makubwa kwenye kutibu vidonda vya tumbo. Majani haya ni Asili na yanatumika kwa wiki mbili tu. kadiri unavotumia utaanza kuona mabadiliko na hatimaye kupona.
Majani haya ya chai yamehifadhiwa katika box moja lenye pakiti 16 na itatumika kwa kipindi siku 16. Majani ya chai yametengenezwa kwa kuzingatia uasili wake pasipo kuwa na kemikali. Kama wewe ni muumini wa vitu asili basi usiache kutumia chai hii ya in-cleansing. Na Vidonge vipo 60 utameza 2×1 kila siku.
Lishe ya Mgonjwa wa vidonda Vya Tumbo
Ifuatayo ni list ya vyakula ambavyo unaweza kutumia ili kupata nafuu ya haraka kutokana na tatizo la vidonda vya tumbo.
- Kula kiasi kidogo kidogo cha chakula kila mara: hii itapunguza makali ya vidonda vya tumbo na pia uwepo wa tindikali kwenye vidonda.
- Tumia vyakula vyenye kambakamba(fibers) kwa wingi: tumia walau gramu 30 za vyakula vyenye kambakamba kwa siku. Vyakula hivi ni kama parachichi , nafaka isiyokobolewa na mboga za majani. NB kama ulaji wa chakula Fulani kinaongeza tatizo basi usitumie, na pia kama dactari wako ameshauri usile chakula fulani kutokana na mwenendo wa tatizo lako basi usile.
- Tumia juisi ya kabeji kila siku: Tafiti mbalimbali zinzonesha kwamba juisi ya kabeji ina uwezo mkubwa wa kutibu vidonda vya tumbo, unaweza ukachanganya na karoti.
Vyakula vya kuepuka kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
- Vyakula vilivyoongezwa ladha au viungo, hufanya tatizo kuwa kubwa zaidi
- Vyakula vyenye Caffeine kwa wingi kama kahawa, na baadhi ya chai (siyo zote)
- Pombe na sigara
- Vyakula vyenye sukari, vyaweza kuwa chakula cha bacteria na kufanya tatizo lako kuwa baya zaidi.