Historia Ya Ugonjwa Wa Ukimwi, Elimu Ya Kinga Na Tiba.
Ukimwi ni ugonjwa unaosambazwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia majimaji au damu yenye virusi. Virusi vya Ukimwi hushambulia seli za CDS ambazo hitwa T cells na kuzorotesha kinga ya mwili kadiri athari inavoongezeka. Kazi ya T cells ni kusaidia Mwili kupambana na maradhi.
Kumbe kadiri Maambukizi ya ukimwi yanavosambaaa kwenye mwili pasipo mgonjwa kutumia dawa ndivyo kinga inavoshuka zaidi. Kinga ya mwili inaposhuka kwa kiasi kikubwa hupelekea mwili kushambuliwa kirahisi na magonjwa nyemelezi (oppotunistic infections) kama saratani, kifua kikuu, fangasi na mengine mengi.
Takwimu Za Ugonjwa Wa Ukimwi barani Africa.
Ukimwi unasababisha vifo vya watu karibu 6,000 kila siku barani Africa. Eneo la kusini mwa jangwa la sahara ndilo eneo lililoathiriwa zaidi na Janga la ukimwi, theluthi mbili ya wagonjwa wote duniani wanapatikana eneo hili.
Ukimwi Ulianzia Wapi?
Wanasayansi katika utafiti wao waligundua kwamba kuna aina fulani ya nyani wanaopatikana Africa ya kati ndio chanzo cha Ukimwi duniani. Na inaaminika kwamba binadamu wa zamani waliambukizwa ukimwi na nyani hawa wakati wanawinda na kula nyama zao. Kwa miaka kadhaa sasa ugonjwa huu umekua kwa kasi mno na kusambaa duniani kote.
Ukimwi Unaambukizwaje Kutoka Kwa Mtu Mmoja Kwenda Kwa Mwingine?
Njia zifuatazo zinaaminika kusambaza virusi vya ukimwi kutoka kwa mgonjwa mpaka kwa mtu mzima.
- Kufanya ngono isiyo salama na mtu mwenye maambukizi ya VVU. Wanaofanya ngono kinyume na maumbile wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa kuliko wanaofanya ngono kupitia uke
- Kuchangia vyombo vyenye ncha kali mfano sindano na vifaa vinavyotumika kuandaa dawa. NB ili mtu kuambukizwa VVU ni mpaka damu ya mgonjwa igusane na kidonda ama mchubuko wake
- Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua. Hii inatokea mara chache kwa sasa kutokana na kwamba matumizi ya dawa za ART zinasaidia sana kupunguza hatari ya kusambaa kwa VVU kwenda kwa mtoto.
- Kufanya ngono kwa mdomo
- Kupata damu kutoka kwa mgonjwa mwenye VVU
Imani potofu kuhusu ukimwi
Kumbuka huwezi kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwenye njia hizi
- Kuvuta hewa ya mgonjwa au kuchangia maji ya kunawa na kuoga na mgonjwa wa VVU
- Kubusu, kugusa mate, machozi na jasho la mgonjwa wa VVU
- Kungatwa na mbu aliyemuuma mgonjwa wa VVU
- Kuchangia choo, chakula au vinywaji na mgonjwa wa VVU
Hatua Za Ukuaji Wa Ugonjwa Wa Ukimwi Kwa Mwathirika
Pale mtu anapopata maambukizi ya virusi vya ukimwi VVU na asipate huduma ya dawa mapema basi anapitia hatua tatu za ukuaji wa ugonjwa. Tiba ya kupunguza makali ya ukimwi-Anti retroviral therapy-ART husaidia kudumaza virusi vya Uimwi na vinamsaidia mgonjwa wa stage yoyote ya gonjwa. Matumizi sahihi ya vidonge hivi hupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa na pia kupunguza hatari ya kusambaa kwa ugonjwa kwenda kwa mtu mwingine.
Hatua ya kwanza: Acute HIV infection
Hatua hii ni ndani ya week 2 mpaka 4 baada ya kupata maambukizi. Mgonjwa anaweza kupata dalili za mafua ambayo huchukua wiki kadhaa kuisha. Watu waliopo katika hatua hii ya mwanzo ya maambukizi wana kiwango kikubwa cha virusi vya ukimwi lakini wengine wao wanakuwa bado hawajui kama tayari wameambukizwa.
Vipimo kama ”fourth-generation antibody/antigen test” na Nucleic Acid (NAT) vinaweza kutumika kugundua maambukizi ya awali . Hivo kama una wasiwasi kwamba unaweza kuwa umeambukizwa Ukimwi kwa kupata mafua ya muda mrefu yanayoambatana na homa basi fika kwenye kituo cha afya uweze kupata vipimo.
Hatua ya pili: Clinical latency (HIV inactivity or domancy)
Kipindi hiki huitwa pia asymptomatic HIV infection au chronic HIV infection. Ndani ya kipindi hiki mtu mwenye VVU haoni dalili mbaya za ugonjwa. Virusi wanakuwepo lakini wanazaliana kwa kasi ya chini sana. Kipindi hiki kinaweza kuchukua hata miaka 10 kwa baadhi ya watu.
Ikumbukwe kwamba ndani ya kipindi hiki uwezekano wa mtu mwenye VVU na hatumii dawa za ARV kumwambukiza mtu mwingine ni mkubwa sana ukilinganisha na wale wanaotumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi. Baada ya hatua hii kiwango cha virusi ndani ya mwili huanza kuongezeka kwa kasi sana na mgonjwa huanza kupata dalili kali za ugonjwa.
Hatua ya 3:Acquired immunodeficiency syndrome (AIDS)
AIDS ni muunganiko wa magonjwa nyemelezi ambayo humpata mtu mwenye Virusi vya Ukimwi (VVU) baada ya kinga ya mwili kushuka sana. Hii ni hatua mbaya zaidi katika kusambaa kwa ugonjwa wa Ukimwi. Bila matibabu mgonjwa wa Ukimwi anaweza kuishi si zaidi ya miaka mitatu na kufa. Kufikia hatua hii vipimo huonesha kiwango cha seli za CD4 chini ya seli 200 kwa mililita. watu wenye magonjwa nyemelezi huwa na kiwango kikubwa sana cha virusi vya ukimwi kwenye damu.
Nitajuaje Kama Tayari Nimeambukizwa Ukimwi?
Njia moja sahihi kabisa ya kupata uhakika kama tayari umeambukizwa ni kufanya vipimo. Kujua hali yako ya kiafya ni muhimu zaidi kwani itakusaidia kufanya maamuzi sahihi ili kuepusha kusambaza ukimwi kwa wapendwa wako.
Baadhi ya watu wanaweza kupata dalili za mafua yanayoambatana na homa ndani ya week 2 mpaka 4 za mwanzo baada ya kupata maambukizi ya Ukimwi. Wagonjwa wengne hupata dalili kama
- Kupata jasho jingi wakati wa usiku
- Maumivu ya misuli
- Mwili kufa ganzi na kuchoka sana
- Kuvimba kwa tezi kwenye kwapa
- Vidonda kwenye mdomo
- Kukauka kwa koo
Kama unapata dalili hizi haimaanishi kwamba sasa una Ukimwi. Dalili hizi zinaweza kusababishwa pia na magonjwa mengine na siyo ukimwi tu. Ndio maana tunasisitiza umuhimu wa kufanya vipimo hospitali au kituo cha afya.
Magonjwa Nyemelezi
Magonjwa nyemelezi ni muunganiko wa magonjwa yanayompata mwathirika wa Ukimwi kutokana na kushuka kwa kinga yake ya mwili. Kwa wagonjwa wenye VVU na wanendelea na dawa za kupnguza makali ya ugonjwa wanapunguza hatari ya kupata magonjwa haya nyemelezi. Watu wengi wanaoshambuliwa na magonjwa haya ni eidha bado hawajui kama wana virusi vya ukimwi ama wanajua lakini bado hawajaanza kutumia dawa za ARV.
Kwa maelezo haya basi kuna umuhimu kwa wagonjwa wa Ukimwi kuyafahamu vyema magonjwa nyemelezi. Hii itakusaidia kushirikiana vyema na mtoa huduma katika kupambana na maradhi yako.
Magonjwa nyemelezi yanayoathiri zaidi wagonjwa wa Ukimwi.
Fangasi kwenye koo la hewa, umio la chakula na mapafu:
Maambukizi haya husababishwa na fangasi wa candida. Mambukizi ya fangasi hawa yanaweza kuathiri viungo kama kucha, ngozi, tishu zenye maji maji kote mwili hasa mdomoni na ukeni. Watu wenye VVU hupata fangasi za mara kwa mara kwenye uke, mdomoni na pia kwenye tishu za mapafu.
Saratani ya shingo ya kizazi
Kansa hii yaweza kuanzia kwenye shingo ya kizazi na kusambaa kwenye maeneo mengine ya uzazi. Saratani hii inaweza kuzuiwa kwa kufanya vipimo mara kwa mara ili kutibu tatizo mapema.
Kaposi’s Sarcoma
Aina hii ya saratani husababishwa na virusi wanaoitwa kaposi’s sarcoma herpevirus ambapo hufanya mirija midogo ya damu kukua kusiko kawaida. Saratani hii yaweza kutokea mahali popote kwenye mwili maana mishipa ya damu iko pote mwilini. Ugonjwa unaweza kuwa hatari zaidi pale unapoathiri viungo muhimu vya mwili kama mapafu, tezi na utumbo.
Tuberclosis (TB):
Mambukizi ya kifua kikuu (TB) husababishwa na bacteria wa Mycobaterium tuberclosis. TB inaweza kusambazwa kupitia njia ya hewa, kama mtu mzima akivuta hewa ya mwathirika. Baadhi ya dalili za Tb ni pamoja na kupata kikohozi kisichoisha, chafya isiyoisha na homa kali,mwili kuchoka sana, kupungua uzito na kupata jasho jingi usiku. Japo ugonjwa unaanzia kweye mapafu lakini unaweza kuathiri mpaka ubongo, mifupa, tezi na figo.
Pneumocystistis carinii pneumonia
Mambukizi haya hutokea kwenye mapafu na husababishwa na fangasi wanaoitwa pneumocystis carinii. Maaambukizi haya hutokea kwa watu wenye kinga hafifu mfano wenye VVU.
Salmonella septicemia
Salmonella ni aina ya bacteria wanaoingia mwilini mwako kupitia chakula na vinywaji. Maambukizi ya Salmonella husababisha dalili kama kutapika, kichefuchefu,homa na kuharisha sana.
Jinsi ya Kuzuia Athari Za Magonjwa Nyemelezi kwa Mgonjwa wa Ukimwi
Njia nzuri ya kujuzuia kupata magonjwa nyemelezi ni kuzingatia huduma ya tiba unayoendelea nayo hospitali. Ikiwemo ushauri juu ya lishe kadiri ulivoelekezwa na dactari. Kwa kuzingatia huduma ya dawa na ushauri utaimarisha afya yako, kuimarisha kinga na kupunguza hatari ya kuwaambukiza watu wengine.
Kumbuka matumizi ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi ni jambo la maisha yote na hutakiwi kukatisha hata siku moja ukishaanza dozi. Kwa kuongezea fuata pia ushauri huu kama tayari unatumia vidonge vya ARV.
Ushauri
- Tumia condom kwa usahihi kwa kila tendo ili kukuepusha na magonjwa mengine ya zinaa
- Usichangie vifaa kama sindano na mtu mwingine. damu inaweza kuwa na maambukizi ya magonjwa ya homa ya ini.
- Hakikisha unapata chanjo kwa magonjwa mbalimbali. Hakikisha unapata mwongozo kutoka kwa dactari juu ya chanjo unazotakiwa kuzipata.
- Fahamu na upate kusoma kuhusu magonjwa gani nyemelezi yanayoweza kukupata na jinsi ya kujikinga na mambukizi haya
- Usinywe maji ambayo hayajatibiwa. hakikisha unakunywa maji safi na salama kila siku.
- Jaribu IMMUNE CARE PACKAGE KUTOKA KWETU yenye mchanganyiko wa virutubisho vilivyo kwenye mfumo wa vidonge aina tatu ambavyo vitakusaidia
- Kuongeza idadi ya seli nyeupe za damu ambazo hupambana na magonjwa nyemelezi kama TB, Fangasi, Pneumonia na kupunguza makali ya VVU
- Kuharakisha uponaji wa vidonda na kuupa mwili nguvu
- Kupambana na saratani zinazoshambulia mgonjwa wa Ukimwi
- Pale virutubisho hivi vinapotumika pamoja na dawa za ARV’s hujenga mwili na Kuimarisha kinga ya mwili hivo kuongeza miaka zaidi ya kuishi kwa mgonjwa wa Ukimwi.
Je kuna Tiba Ya Ukimwi?
Mpaka sasa bado hakuna tiba ya moja kwa moja ya ugonjwa wa Ukimwi. Tiba ya sasa ya Anti Retroviral Therapy inalenga katika kufubaza virusi vya ukimwi (VVU) na kupunguza makali ya ugonjwa.
Dawa hizi zikitumika kwa usahihi kila siku huongeza muda wa kuishi kwa waathirika wa ukimwi, kuimarisha afya zao na Kupunguza hatari ya kuwaambukiza wengine. kwa hivo kadiri utakavopata vipimo haraka na kuanza dawa mapema ndivyo unavoongeza umri wa kuishi.