Kama umewahi kuamka asubuhi na ukajikuta na maumivu makali kwenye dole gumba. Basi fahamu kwamba unapata dalili za ugonjwa wa gout. Tatizo hili kwa miaka ya zamani lilifahamika kama ugonjwa wa wafalme na matajiri (disease of the kings).
Kwa sababu wafalme na matajiri wa zamani walikunywa pombe, kula nyama nyingi pasipo kushugulisha miili yao. Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza ni mmoja ya wafalme waliougua ugonjwa huu. Alexander the great, Christopher columbus, Sir Isaack newton ni baadhi ya watu maarufu ambao waliugua ugonjwa wa Gout.
Lakini sasa hivi mambo yamebadilika hakuna cha mfalme, maskini wala mtu wa kawaida kila mtu yupo kwenye hatari ya kuugua gout. Hii ni kutokana na mabadiliko ya dunia. Kila mtu anaweza kunywa pombe, kula nyama na anasa. Takwimu zinaonesha kwamba idadi ya watu kuugua gout imeongezeka mara mbili kwa kipindi cha miaka 20 sasa.
Gout ni nini hasa?
Gout ni ni ugonjwa wa maungio ya mifupa unaoambatana na maumivu makali sana. Ugojwa huu unasababishwa na mkusanyiko wa uric acid kupita kiasi kwenye joint zako. Mkusanyiko huu hupelekea kufanyika kwa vijimawe vidogo mithili ya sindano-crystals ambavyo ndo vinakuchoma na kuleta maumivu makali.
Uric acid ni zao linapatikana baada ya mwili kuvunjavunja purine inayopatikana kwa wingi zaidi kwenye vyakula kama nyama, samaki, mazao ya vyakula vyenye nundu (legumes) kama maharage, karanga, pombe, na sukari ya fructose inayopatikana kwenye matunda.
Fikra potofu kuhusu gout
Nimekuwa nikipokea kesi nyingi za wagonjwa kuhusu tatizo la gout na wengi hushauriwa kutokula kabisa nyama. Nataka nikwambie leo adui yako mkubwa siyo nyama bali ni sukari unayokula kupita kiasi. Tunashauri tu usile nyama kutokana na kwamba tayari umeanza kuumwa. ila hili siyo suluhisho la muda mrefu. Uric acid katika hali ya kawaida ya mwili siyo kitu kibaya kama mwili unafanya kazi kikawaida na figo zako ziko vizuri itasafirshwa kwenye damu na kisha kutolewa nje kama mkojo.
Tatizo linakuja pale uric acid inapozidi kupita kiasi ama figo zako zikawa hazifanyi kazi vizuri ndipo vijimawe hivi kama sindano huanza kujitengeneza kwenye joint na kuanza kuchoma na kusababisha maumivu makali zaidi.
Kama hutabadilisha lishe yako na kupata tiba inayolenga kutatua chanzo cha tatizo basi kuna uwezekano ukaugua tena na tena gout. Kila siku huwa nasema lishe ndio mchawi wa matatizo yetu, ukijua tu button ya kubonyeza kwenye lishe basi hutasumbuka na magonjwa mengi sana.
Dalili na Viashiria kwamba una Gout
Kwa wagonjwa wengi maumivu huja na kuondoka na kisha kurudi tena baada ya week ama siku kadhaa. Kwa wengine maumivu huwa ya kila siku. Kikawiada maumivu huwa makali sana ndani ya masaa 12 mpaka 24 baada ya kupatwa na ugonjwa. Uafadhali unakuja kutokana na lishe na dawa unazomeza. Ukiachilia mbali maumivu kwenye dole gumba la mguuni ambayo ni dalili kuu. Dalili zingine ni kama
- Maumivu kwenye joints hasa kwenye miguu, enka, magoti, hips,mikono, vidole kiasi kwamba hata kubeba shuka na nguo itakuwa shida kwako.
- Kupishana kwa joints na kuwa na rangi nyenkundu na purple
- Kuvimba kwa maungio ya mifupa na ngozi yake kuuma sana kiasi kwamba hata ukigusa panawaka kama moto
- Homa kali na joto kupanda hadi kufikia 39c
- Joint kuvimba na kuwa laini sana: Kadiri ugonjwa unavokaa muda mrefu hutengeneza vifundo ambavyo huleta maumivu makali zaidi na kuharibu joints zako na hata mpangilio wa mifupa. Ni muhimu sasa kumwona daktari wako unapofikia hatua hii mbaya ili upate usaidizi wa kiafya.
Tiba ya Kisasa kwa Tatizo la Gout
Matatizo yaliyo mengi ya gout huondolewa kwa kutumia dawa. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs), colchicine au corticosteroids hutumika kuondoa maumivu kwenye eneo lililoathirika na gout. Japo mgonjwa atakuwa mteja wa dawa hizi miaka yote maana zinalenga katika kutibu dalili na siyo chanzo cha tatizo.
Vyakula aina 6 Asilia Vitakusaidia Kutibu na kuzuia Gout.
Ugonjwa wa gout unaletekezwa kwa kiasi kikubwa na lishe. Kwahiyo ukibadilisha baadhi ya vyakula utapunguza makali ya ugonjwa na kuondoa atari ya tatizo kujirudia siku za mbele.
- Tumeric au manjano.
Manjano ni kiungo tiba cha miaka mingi ambacho kimekuwa kikitumiwa tangu enzi za zamani kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya moyo na gout. Unaweza kutumia unga wake vijiko viwili mara tatu kwa siku. - Kahawa: unywaji wa kahawa mara kwa mara inaaminika kupunguza kiwango cha uric acid mwilini.
- Vyakula vyenye kambakamba kwa wingi kama viazi. ndizi, mboga za majani na parachichi.
- Vyakula vyenye magenesium kwa wingi kama mbegi za maboga, mtindi, parachichi, broccoli na almonds
- Lishe yenye vitamin C kwa wingi kama: Machungwa, hoho, broccoli, mapera na straberries.
- Vyakula vyenye mafuta ya omega 3 kwa wingi kama samaki. Unaweza pia kutumia virutubisho kama deap sea fish oil kama tayari unaumwa ili kukusaidia kupata nafuu haraka.
Mazingira Hatarishi na sababu zinazokufanya Uugue Gout
- Lishe
Ulaji wa vyakula vyenye purine kwa wingi kama pombe na sukari ya fructose inayopatikana kwa wingi kwenye soda na vinywaji vya kusindika. - Uzito mkubwa na kitambi
Watu wenye uzito mkubwa na kitambi hutengeneza uric acid kwa wingi na figo kushindwa kutoa acid mwilini. Metabolic syndrome ni tatizo linatokea kwa shughuli za mwili kutoenda inavotakiwa. Matatizo kama uzito mkubwa kupanda shinikizo la damu na insulini huletekezwa na metabolic syndrome na chanzo kimojawapo cha metabolic syndrome ni kuongezeka kwa uric acid kwenye damu . - Wagonjwa wenye historia ya kupata matatizo ya kiafya hapo nyuma:
Watu wenye matatizo ya kiafya kama kisukari, shinikizo kubwa la damu, magonjwa ya moyo, na matatizo ya cholesterol nyingi wapo kwenye hatari zaidi ya kupata gout. - Magonjwa ya figo: kama tulivyosoma pale juu figo ni kiungo muhimu kwenye utoaji wa uric acid, hivo figo inapopata hitilafu, kiwango kingi cha uric acid kitajikusanya kwenye maungio ya mifupa na kutengeneza vijimawe.
Maelezo ya Mwisho kwa wewe Mgonjwa wa Gout
- Gout ni ugonjwa hatari unaweza kuletekeza ulemavu wa viungo ambao unaweza kukupata haraka pasipo kutoa vashiria
- Gout huwapata zaidi wanaume kuliko wanawake
- Kurekebisha lishe na kuepuka vyakula kama pombe na sukari ni njia ya kuanzia katika kutibu tatizo lako
- Gout isipotibiwa na kuwa chronic hutengeneza vifundo na kubadilisha kabisa mwonekano wa viungo vyako hata ukashindwa kutembea na kufanya kazi
- Kuwa na Gout kunakuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa zaidi ya figo na moyo
- Kufanya mazoezi mara kwa mara husaidia kutoa sumu ya uric acid kwenye damu: tumia hii kama njia ya kuzuia na siyo kutibu maana ni vigumu kufanya mazoezi wakati unaumwa utashindwa.
- Kula zaidi vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi
Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, hii itakusaidia si tu kuondoa hatari ya kupata gout bali hata kuweka sawa shinikizo la damu na kuzuia magonjwa ya figo - Anza kwa kutumia virutubisho hivi asili kutoka kwetu, kusafisha figo, na kuondoa uric acid iliyojikusanya kwenye maungio ya mifupa.
Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai.