Shinikizo kubwa la damu ni hatari kwasababu inaweza kuletekeza kifo cha bila kutegemewa, ukiacha hatari zingine ambazo mgonjwa anakuwa nazo kama kupata kiharusi, shambulizi la moyo, moyo kushindwa kufanya kazi na matatizo ya figo.
Je wafahamu kwamba watu wengi wenye presha kubwa ya damu hawatambui kwamba wana tatizo na hawaoni dalili zozote mbaya mpaka wanakuja kufanya vipimo. Habari nzuri ni kwamba unaweza kuzuia tatizo hili kwa kuzingatia lishe na kurekebisha mfumo wako wa maisha.
Shinikizo la Damu tunaweza Kugawanya katika Makundi haya
- Normal: chini ya 120/80 mm Hg
- Kiwango cha presha kupanda: 120/80 mm HG mpaka 130/89 mm Hg
- Kiwangu cha juu zaidi: 140/90mm Hg
Kikawaida hakuna dalili zinazojionesha endapo shinikio lako la damu ni kubwa kupita kiasi ila kuna viashiria kadhaa ambayo vinaweza kukupa alam kwamba kuna shida mfano maumivu ya kifua, maumivu ya kichwa, kelele kwenye masikio, kubadilikabadilika kwa mapigo ya moyo, kutokwa na damu puani, uchovu mara kwa mara na kupungua uwez wa kuona.
Mpaka viashiria hivi vikianza kujitokeza ni kwamba presha yako ya damu imefikia pabaya sana.
Nini Kinasababisha Presha kupanda kupita kiasi.
Kumbuka ukifahamu chanzo cha tatizo ni rahisi kutibu na kurekebisha shinikizo la damu. Vitu vingi vinaweza kupelekea shinikio kubwa la damu ambavyo ni pamoja na
- Uzito mkubwa na kitambi :uzito wako unavoongezeka zaidi ndivyo hataru ya kupata presha kubwa ya damu huongezeka hii ni kutokana na uhitaji mkubwa wa damu katika kusafirisha chakula hewa mwilini.
- Umri: kuugua presha kunaongezeka kadri umri unavoongezeka. Wanaume huugua zaidi wakiwa na miaka 45 na kuendelea na wanawake wanaugua zaidi wakiwa na miaka kuanzia 65.
- Kutokushugulisha mwili: watu wasiofanya mazoezi na kushugulisha miili yao, mapigo ya moyo huenda kasi sana na hivo kupelekea shinikizo la damu kuwa juu. Kukosa mazoezi pia huchangia kuongezeka uzito.
- Matumizi ya pombe na sigara: kemikali zilizopo kwenye tumbaku zinaharibu mishipa ya damu ya kuifanya kuwa migumu na hivo mishipa kuwa miyembamba na kupelekea presha ya damu kuongezeka, pombe pia ni kihatarishi kwa shinikizo la damu.
- Msongo wa mawazo na baadhi ya matatizo sugu kama magonjwa ya figo , kisukari na kukosa usingizi.
Madhara ya Presha kubwa ya Damu.
Shinikizo kubwa la damu linaongeza hatari ya kupata changamoto zingine nyingi za kiafya kama
- Shambulizi la moyo
- Kiharusi
- Moyo kuacha kufanya kazi
- Matatizo ya macho kama presha ya macho
- Kisukari, uzito mkubwa na kitambi na mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu na
- Kupasuka kwa mishipa midogo ya damu
Mpangilio wa lishe ili kupunguza hatari ya Kupata shinikizo kubwa la damu.
Vyakula vya kupunguza ili kuepusha hatari ya shinikizo kubwa la damu ni pamoja na
- Pombe
- Vyakula vyenye madini ya sodium kwa wingi mfano chumvi.
- Mafuta mabaya kama mafuta ya pamba, canola, margarine ambayo mengi hupatikana kwenye vyakula vilivyosindikwa.
- Vyakula na vinywaji vya sukari
Vyakula vya Kutumia mara kwa mara ukinywa mgonjwa wa Presha
- Vyakula vyenye madini ya potasium kwa wingi kama madafu, parachichi, ndizi mbivu na tikiti maji
- Vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi kama mboga za majani, matunda, mbegu na maharage.
- Vyakula vyenye mafuta ya omega 3 kwa wingi kama nyama, chia seeds na mbegu za maboga.
Chai ya Kuding itakavyokutibu tatizo lako la Presha
Chai ya kuding imetengenezwa kwa mimea ya Folium camellia, Ganoderma, na Radix Panacis Quinquefolli ni maarufu kwa nchi za wenzetu katika kutibu tatizo la presha. Huna haja ya kumeza vidonge ambayo vina madhara ya muda mrefu , tumia chai ya kuding inayojitosheleza. Chai ya kuding itasaidia
- Kupunguza mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu na hivo kurekebisha presha ya damu.
- Kurekebisha sukari na kupunguza uzito mkubwa na kitambi
- Kusafisha mwili na kuimarisha kumbukumbu
- Chai ya kuding inawafaa watu wote isipokuwa wajawazito