Cholesterol ni nini?
Cholesterol ni vitu vyenye mwonekano wa mafuta ambavyo hutengenezwa na ini kwa ajili ya kusaidia ufanyaji kazi wa seli za mwili, homoni na neva. Mwilini kuna cholesterol nzuri na ile mbaya.
Cholesterol ni muhimu sana kwenye mwili. Lakini kiwango chake kinapozidi ni hatari kwani mafuta haya yaaweza kuziba kwenye mirija ya damu na kupunguza mzunguko wa damu kwenda kwenye viungo muhimu vya mwili. Mafuta haya yanapozidi kujikusanya kwenye mirija ya damu huongeza hatari ya kupata shambulizi ya moyo(heart attack) au kiharusi(stroke).
Je nini Kinasababisha Cholesterol kuwa Nyingi?
Amini usiamini jibu ni tofauti kabisa na wengi wanavodhani kwamba kula vyakula vyenye mafuta ndio chanzo. Kwanza tujue aina za cholesterol.
Aina za cholesterol
Kuna aina mbili za cholesterol, high density lipoprotein(HDL) ambayo ni cholesterol nzuri na low density lipoprotein(LDL) -cholesterol mbaya.
LDL ikiongezeka zaidi huleta hatari ya magonjwa kama shambulizi la moyo na stroke.
HDL-cholesterol nzuri husafiri ndani ya damu. Kazi yake ni kuondoa LDL-mafuta mabaya na kusaidia kulinda afya ya mishipa ya damu na damu iweze kusafiri vizuri. Kumbe ili uonekane na afya njema yatakiwa kiwango cha HDL kiwe kikubwa zaidi kuliko LDL.
Hatari za cholesterol kupanda kwenye damu
Kama tulivosoma mwanzo mwili unahitaji sana cholesterol katika shughuli zake,japokuwa cholesterol mbaya inapozidi hapo shida inaanza. Mishipa ya damu inapungua kipenyo chake pale mafuta mabaya yanapojikusanya kwa ndani an hivo kufanya mzunguko wa damu kuwa mgumu.
Endapo mafuta yataendelea kujikusanya kwenye mishipa kwa mda mrefu unaweza kupata shambulizi la moyo au hata stroke. Hii ni kwa sababu mzunguko wa hewa unapungua kuelekea kwenye moyo na ubongo.
Pamoja na kwamba mwili wako una tabia ya kusafisha cholesterol mbaya kwenye mishipa, ulaji wa vyakula vibovu hasa vyenye mafuta ya kusindikwa yanapunguza uwezo huu wa mwili. Na hivo kupelekea cholesterol mbaya kupanda kupita kiasi.
Nini kifanyike ili kupunguza mafuta mabaya?
Kumbuka kwamba ufanyaji kazi wa aina hizi mbili za cholesterol ni tofauti kabisa. Cholesterol nzuri ya HDL yenyewe inasafiri kwenye mishipa ya damu na kusafisha mafuta mabaya. lakini ile cholesterol mbaya-LDL yennyewe haina tabia ya kusafiri, bali inaganda na kuanza kuziba mshipa wa damu.
Je ni jinsi gani upunguze kiwango cha LDL na uongeze HDL ili kuimarisha afya ya moyo wako? Hii ndio mada yetu ya leo, endelea kusoma zaidi.
Jinsi ya kupunguza Cholesterol mbaya Mwilini
(vyakula vya kutumia kwa wingi)
- Mafuta ya zeituni
Tafiti zimegundua kwamba matumizi ya mafuta ya zeituni(olive oil) mara kwa mara husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini. - Mboga za majani
Mbogamboga zimejaa madini, vitamini na kambakamba(fibers). Matumizi ya mboga za majani mara kwa mara hupunguza mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu. - Karanga
Karanga zimejaa mafuta mazuri na kambakamba, sababu hizi mbili pekee zinakufanya uchague karanga na jamii zake kama chakula cha muhimu. - Mbegu za maboga
- Vitunguu saumu
- Tafiti zinasema kutafuna vitunguu saumu mfululizo kwa miezi miwili hupunguza hatarai ya kupata magonjwa ya moyo kwa kiasi kikubwa.
- Parachichi: Matunda haya yana madini ya potasimu, kambakamba na mafuta mazuri ambayo husaidia kurekebisha cholesterol mwilini.
Vyakula vya kuepuka
Ni muhimu sasa kusafisha jiko lako na kuondoa vyakula sumu vinavyokufanya uwe na cholesterol nyingi kupita kiasi. Vyakula hivi ni kama
- Sukari na Wanga uliochakatwa na kusafishwa
- Pombe
- Caffeine
Matumizi makubwa ya vinywaji vyenye caffeine nyingi kama kama kahawa, soda na energy drinks inaweza kuongeza cholesterol.
Virutubisho vya Kutumia kwa Mgonjwa wa Cholesterol ili kuepuka dawa za hospitali zenye madhara.
1.Chitosan
Chitosan husaidia kupunguza mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu
Kurekebisha sukari kwenye damu, Kuimarisha uwezo wa ini na kuzuia athari za sumu kwenye ini.
2.Garlic oil softgel
Inasaidia kupunguza cholesterol mbaya kwenye mishipa ya damu,
kurekebisha shinikizo la damu na kulinda mfumo wa damu na
Kuzuia magonjwa ya moyo.
Gharama zote kwa tiba ya kusafisha cholesterol mbaya mwilini ni Tsh 150,000/= Dozi ya mwezi mmoja tu. Pia dawa zitakukinga dhidi ya magonjwa ya moyo kama presha na kutanuka moyo.