Saratani ya tezi dume ni ugonjwa hatari unaoathiri maelfu ya wanaume duniani kote kila mwaka. Tezi dume ni kiungo kidogo kinachopatikana chini ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija wa kutoa mkojo (urethra).
Tezi dume inaratibiwa na homoni ya testosterone na kazi ya tezi dume ni kutengeneza majimaji-semen. Majimaji haya huchanganyika na mbegu za kiume ili kuzisaidia kuogelea vizuri kuelekea kizazi cha mwanamke wakati wa tendo la ndoa. Katika makala hii tutaangalia kiundani saratani ya tezi dume inaanzaje na hatua za kuchukua ili kutibu saratani yako kabla hujafanyiwa upasuaji.
Saratani Ya Tezi Dume ni Kitu Gani
Tezi dume imeundwa kwa seli, inapotokea seli hizi zinakua pasipo kuratibiwa vizuri na kutengeneza seli za saratani ndipo tunaita saratani ya tezi dume. Saratani hii inaweza kujitanua na kukua kuelekea maeneo ya karibu kama haitatibiwa mapema.
Aina za Saratani ya Tezi Dume
Saratani ya tezi dume tunaiweka katika kundi la saratani zinazotokea kwenye tishu za tezi (adenocarcinoma). Saratani ya tezi dume hugawanywa kwa kuzingatia kasi ya ukuaji wake
Aina ya kwanza: Aggressive au fast growing ambayo hukua na kusambaa haraka na kuathiri viungo vingine vya mwili kama mifupa
Aina ya pili: Non aggresive au slow growing ambayo hutokea sehemu moja na yaweza kukua taratibu sana au kutosambaa kabisa.
Nini Kinasababisha Upate Saratani ya Tezi Dume?
Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imetambulika kusababisha saratani ya tezi dume lakini kuna muunganiko wa vihatarishi vingi ambavyo tunaviongelea hapa chini.
Makundi yafuatayo yapo kwenye hatari ya kupata saratani ya tezi dume
- Wazee na wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 na kuendelea
- Watu walio kwenye familia yenye historia ya kuugua tezi dume
- Wenye uzito mkubwa na kitambi
- Mazingira hatarishi kama ya mionzi huongeza hatari ya kupata tatizo.
Dalili za Saratani ya Tezi dume
Saratani aina ya pili ambayo ni non aggressive inaweza kutoonesha dalili zozote kwa siku za awali. Lakini pale unapoanza kuona dalili zifuatazo basi hakikisha unamuona daktari mapema ili kufanya vipimo.
Kumbuka pia baadhi ya dalili za saratani ya tezi dume zinaingiliana na dalili za magonjwa mengine kwahiyo ni muhimu kufanyiwa vipimo haraka. Dalili za saratani ya tezi dume ni kama zifuatazo
- Matatizo ya mkojo: matatizo ya mkojo ni kutokana na kwamba tezi hii ipo karibu na mrija wa kutolea mkojo na pia karibu na kibofu cha mkojo. Uvimbe wa saratani unapokua unabinya kibofu na njia ya mkojo na kuletekeza maumivu makali wakati wa kukojoa, kukojoa kila mara, mkojo kutoruka mbali na kupata mkojo wenye damu (hematuria).
- Kukwama kwenye tendo la ndoa: Uume kushindwa kusimama na kukosa kabisa hamu ya tendo la ndoa ni moja ya masaibu yanayowapata wanaume wenye saratani ya tezi dume. Kwani hawapati kabisa matamanio kwa wake zao kiasi cha kuwaona kama ni jinsia moja. Dalili ingine ni kutoa shahawa zinazoambatana na damu.
- Maumivu makali na kupata ganzi: Saratani ya tezi dume inapoanza kusambaa kuelekea kwenye viungo vingine kama mifupa huleta maumivu makali kwenye eneo la nyonga, maumivu nyuma ya mgongo na maumivu ya kifua
- Kama saratani ikisambaa kufikia kwenye uti wa mgongo yaweza kupelekea kushindwa kuhisi kitu kwenye upande wa chini miguuni na kwenye kibofu cha mkojo.
Maelezo ya Muhimu kuhusu Dalili za Saratani ya Tezi dume
Mpenzi msomaji unatakiwa kufahamu kwamba kupata matatizo ya mkojo ndizo dalili za awali kabisa kwamba una shida kwenye tezi yako. Ni muhimu kuweka akili kwamba dalili hizi inaweza kuwa ni kiashiria cha matatizo mengine kama BPH (kukua kwa tezi dume) na Prostatitis ambayo ni maambukizi kwenye tezi dume.
Vipimo ili Kugundua Uwepo wa Saratani ya Tezi dume.
Daktari wako anaweza kukufanyia vipimo vifuatavyo baada ya maongezi na maelekezo jinsi vipimo vinavyofanya kazi.
1.Digital rectal examination (DRE)
Kwa kipimo hiki daktari ataingiza kidole chake kilichovalishwa gloves kwenye sehemu yako ya haja kubwa ili kutambua uwepo wa tishu ngumu ama uvimbe wa tezi dume ambao unaweza kuashiria uwepo wa saratani.
2.Prostate specific antigen (PSA test)
Kipimo hiki kinaangalia kiwango cha protini ya PSA kwenye damu. Kma una kiwango kikubwa cha PSA basi kuna hatari kwamba una saratani ya tezi dume.
3.Prostate Biobsy
Daktari anaweza kuhitaji kiwango cha tishu za tezi dume na kufanyiwa vipimo maabara ili kugundua uwepo wa saratani. Kiwango kidogo cha nyama ya tezi dume hupelekwa maabara ya kupimwa.
4.Vipimo vingine ni utrasound, MRI na CT scan, vyenye uwezo wa kuchukua picha za ndani ya mwili na kugundua uvimbe.
Tiba ya Saratani ya Tezi dume
Kwa kuangalia hali ya yako ya kiafya, umri wako na hatua ya saratani yako, daktari atatengeneza mpangilio mzuri wa tiba inayokufaa.
Kama aina yako ya saratani ni ile non aggresive ambayo haikui na kusambaa kwenda sehemu zingine za mwili, ndipo utakuwa chini ya uangalizi (active surveillance). Kwa kufanyiwa vipimo mara kwa mara pasipo kuanzishiwa huduma ya tiba.
Kwa Saratani ambayo ni tishio inayosambaa kwa haraka (aggresive) inaweza kutibiwa kwa njia hizi
- Upasuaji kuondoa kabisa tezi dume: ambapo mwanaume hataweza kupata tena hamu ya kufanya tendo la ndoa.
- Tiba ya mionzi (radiation)
- Tiba kwa kutumia homoni (hormone therapy)
- Chemotherapy
Je kuna Uwezekano wa Kupona Kwa mgonjwa wa Saratani ya Tezi dume.
Kama saratani yako itagundulika mapema kabla haijasambaa kutoka ilipoanzia matokeo ya kupona ni makubwa. Ugunduzi wa saratani mapema na kuitibu mapema ndio silaha nzuri inayoongeza matumaini ya kupona saratani hii.
Kwahiyo kama unafikiri unaona kuona dalili za uwepo wa saratani ya tezi dume, hakikisha unamwona daktari haraka ili uanze tiba ya tatizo lako mapema.
Jinsi ya Kuzuia na Kupunguza hatari ya kupata Saratani ya Tezi dume.
Baadhi ya vihatarishi kama umri tunajua ni vigumu kuzuia lakini baadhi ya mitindo ya maisha unaweza kurekebisha kama kuacha kuvuta sigara, kufanya mazoezi na lishe nzuri.
Lishe yenye vyakula hivi inaaminika kuzuia na kupunguza hatari ya kupata saratani ya tezi dume. Vyakula hivi ni pamoja na nyanya, mboga kama Broccoli, samaki na mafuta ya samaki yenye omega 3 kwa wingi kama mafuta ya mizeituni.
Utafiti unasemaje Kuhusu Tiba ya Mimea ya Wachina (Chinese Traditional Medicine-TCM)
Tiba hii ambayo imeanza kutumika kwa kwa zaidi ya miaka 5000 sasa kwenye kutibu magonjwa ya tezi dume ikiwemo saratani ya tezi dume, mambukizi kwenye tezi dume (prostatitis), na ukuaji usio wa kawaida wa tezi dume (BPH).
Ni wazi kwamba nchi za wenzetu kama China, Korea na Thailand idadi ya wanaume wanaougua tezi dume ni wachache sana. Hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya dawa hizi za mimea ambazo nitazielezea kwa kina hapa chini ili nawe uanze kuzitumia.
1.Prostacare
Prostare imetengenezwa kwa viungo vya Anemarrhenae, Cortex Phellodendri Chinsis, Herba Ecliptae, Fructus na Ligustri Lucidi.
Dawa itakusaidia
- Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya tezi dume
- Kuzuia kuzaliana kwa wadudu wabaya ndani ya tezi dume
- Kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume
- Kuondoa seli za tezi dume zilizokufa na kutibu madhara yatokanayo na kukua kwa tezi dume.
Dawa hii inafaa kutumika zaidia kwa
- Mwanaume mwenye tatizo lolote la tezi dume
- Wanaume wenye umri unaozidi miaka 40
- Dawa inagarimu Tsh 100,000/=
2. Lycopene
Viungo:B-Carotene, Lycopene
Kazi Na Faida Zake
- Huzuia kansa na hasa kansa ya tezi dume
- Hufanya kazi kama antioxidant yenye nguvu na kuondoa sumu mwilini
- Lycopene inapunguza mafuta mabaya kwenye damu mishipa ya damu
Yafaa Kutumiwa Na:
- Wanaume wenye matatizo ya tezi dume kama tezi kuvimba na saratani ya tezi dume
- Gharama ni Tsh 75,000/=
3.Ginseng & Ganoderma capsules
Kazi na Faida za Ginseng na Ganoderma
- Kupambana na seli za saratani
- Kupunguza kasi ya ukuaji wa saratani
- Kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya saratani na
- Kupunguza madhara ya chemo na mionzi kama kutapika, uchovu, kukosa hamu ya kula, na nywele kunyonyoka
- Gharama ya Ginseng na Ganoderma ni Tsh 210,000/=
Tafakari
Fikiria kuepusha mamilioni ya pesa za gharama kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa kutumia dawa hizi pekee na ukaepuka tatizo hili la saratani ya tezi dume na kutibu magonjwa yote ya tezi dume.
Fikiria pia kurudisha furaha yako kwenye tendo la ndoa baada ya kutibu saratani ya tezi dume pasipo kufanyiwa upasuaji. Upasuaji ambapo tezi nzima huondolewa nawe usiweze kuwa na matamanio kabisa na mke/mpenzi wako.