Saratani ya matiti

saratani ya matiti

Saratani ni ugonjwa unaotokea kutokana na mabadiliko kwenye chembechembe ndogo sana zinazoitwa gene ambazo hupatikana kwenye seli za mwili. Mabadiliko haya tunaita mutation na husababisha seli kuanza kukua pasipo mpangilio maalumu na kutengeneza seli nyingi ambazo siyo za kawaida.

Kadiri seli hizi zinavokua baadae zinatengeneza uvimbe wa saratani ambao kitaalamu huitwa tumour. Katika makala ya leo tutajikita zaidi katika kuchambua saratani ya matiti.

Saratani ya matiti (Breast Cancer) ni aina ya saratani inayotokea kwenye matiti. Kwa kiasi kikubwa saratani hii hutokea kwenye tezi za lobules ambazo huhusika katika utengenezaji wa maziwa na kwenye mirija inayosafirisha maziwa kutoka kwenye tezi mpaka kwenye chuchu ya titi.

Saratani ya matiti inaweza pia kufanyika kwenye tishu zinazohifadhi mafuta kwenye titi lako. Seli za saratani ambazo tayari sasa zimeathirika huanza kuvamia seli zingine hai.

Wanaume pia Wanaweza Kupata Saratani ya Matiti.

Saratani ya titi siyo kwamba inawatokea wanawake tu bali hata wanaume. Katika kila wagonjwa 100 wa saratani ya titi basi mmoja kati yao anaweza kuwa mwanaume. Wanaume wanaofanya kazi kwenye sehemu za mafuta, kemikali na mionzi  wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani. Mbaya zaidi ni kwamba wengi hugundulika hali ikishakuwa mbaya na ugonjwa umesambaa sana.

Saratani ya Matiti Husababishwa na nini?

Saratani ya titi inatokana na mcharuko(inflammation) unaotokana na mpambano ndani ya titi. Mcharuko huu wa tishu ndio kianzio cha ukuaji wa saratani. Lakini kuna vihatarishi vingi vinavyopelekea kutokea kwa mcharuko huu ikiwa ni vyakula, kemikali na mtindo wa maisha kwa ujumla tunaoishi.

Kumbe tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa kutokea kwa saratani ya matiti kwa kuepuka vihatarishi vinavyopelekea kutokea kwa mcharuko(inflammation). Vihatarishi hivi hupelekea kubadilika kwa mipangilio ya gene kwenye seli na ndipo seli zisizo za kawaida za saratani  huanza kuzalishwa na kukua.

Aina za Saratani ya Matiti.

Saratani ya matiti inagawanywa katika makundi makubwa mawili. Invasive ambayo inasambaa kutoka kwenye tezi za kutengeneza maziwa  na non invasive ambayo inaathiri tu eneo la tishu ambapo imeanzia. Yaani haisambai kuelekea kwenye maeneo mengine ya titi. Makundi haya mawili tunaweza kuyaweka kwenye aina nne za saratani ya matiti ambazo ni

  1. Ductal carcinoma in situ.(DCIS) ambayo ni saratani inayotokea kwenye mirija ya kusafirisha maziwa .saratani hii haisambai na pia inakuwa bado haijaathiri tishu za matiti zilizo karibu.
  2. Lobular carcinoma in situ(LCIS) . ni saratani inayotokea kwenye tezi za kutengeneza maziwa. Kama ilivyo DCIS, saratani hii inakuwa haijasambaa na kuathiri tishu za karibu yake.
  3. Invasive ductal carcinoma(IDC), saratani hii hujitokeza zaidi kuliko aina zingine za saratani. Katika steji hii saratani inaanzia kwenye mirija ya kusafirisha maziwa kwenye kwenye chuchu kisha inasambaa kwenye tishu za karibu na kama tatizo halitadhibitiwa basi saratani hii inaweza kusambaa hadi kwenye viungo vingine vya mwili.
  4. Invasive lobular carcinoma(ILC)– saratani hii inaanzia kwenye tezi za kutengeneza maziwa-lobules na huanza kukua kuelekea kwenye tishu na viungo vya karibu ya titi.

Mazingira Hatarishi Yanayoongeza Uwezekano wa Kupata Saratani ya Matiti.

Kuna tabia na mazingira yanayoongeza uwezekano wa kupata saratani ya matiti. Lakini siyo kwamba sababu moja pekee inaweza kupelekea upate saratani. Baadhi ya Tabia hatarishi zinaweza kuwa ngumu kuepukika kama historia ya ugonjwa kutoka kwenye familia. Mazingira mengine hatarishi ni

  • Umri; wanawake wenye umri zaidi ya miaka 55 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya titi
  • Unywaji wa pombe
  • Wanawake wapo kwenye hatari zaidi mara 100 kuugua saratani ya titi ukilinganisha na wanaume
  • Kuvunja ungo mapema: wanawake wanaovunja ungo kabla ya kutimiza miaka 12 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na wengine
  • Kuanza kujifungua katika umri mkubwa hasa kuanzia miaka 35.
  • Tiba za homoni-hormone therapy; wanawake waliopo kwenye tiba ya homoni za kuchelewesha kukoma hedhi wanaongeza hatari ya kupata saratani ya matiti.
  • Kuchelewa kukoma hedhi: kuanzia miaka 55 na kuendelea
  • Kutozaa kabisa
  • Waliowahi kupata saratani ya matiti kipindi cha nyuma.
  • Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa muda mrefu

Dalili za Saratani Ya Matiti

Saratani inapoanza haioneshi dalili zozote. Mgonjwa anaweza kutambua uwepo wa uvimbe wa saratani kwa kufuata maelekezo ambayo tutatoa hapa chini. Kila aina ya saratani inaweza kusababisha dalili mbalimbali. Dalili zifuatazo ni zile zinazoingiliana

  • Uwepo wa tishu ngumu ambazo ni tofauti na tishu zingine
  • Kupata maumivu kwenye titi.
  • Rangi ya titi kubadilika na kupata wekundu
  • Kuvimba kwa titi
  • Kutokwa na majimaji yasiyo maziwa kwenye matiti
  • Kutokwa na damu wenye chuchu za titi
  • Kupata mabadiliko ya umbo la titi kusiko kawaida
  • Kuhisi uvimbe au nundu kwenye titi

Angalizo: Siyo kwamba ukiona dalili mojawapo kati ya hizi ndio uhakikisho kwamba una saratani ya matiti hapana. Unapopata dalili hizi hakikisha unaenda hospitali kufanya vipimo mapema ili kupata uhakika juu ya tatizo.

Jinsi ya Kugundua uwepo wa Saratani kwenye Titi kwa Kutumia Mkono

Ndugu msomaji napenda basi niguse kidogo njia ambazo unaweza kuzichukua ili kuubaini ugonjwa huu wa kansa ya titi. Zifuatazo ni hatua kwa hatua ambazo unaweza kuzitumia ukiwa nyumbani kwako

Hakikisha unapata historia nzuri ya ugonjwa wako, ili kuweza kutofautisha na uvimbe mwingine wa kawaida. Hakikisha unajichunguza wewe mwenyewe vizuri; Unaweza kumwomba mtu akuchunguze kwa kufuata hatua hizi kuu mbili:

Hatua za kubaini saratani

Njia ya kwanza: Lala kitandani chali, kisha mwambie rafiki yako atumie mkono wake wa kulia kupapasa juujuu na kisha kuingia mpaka ndani. Pia ajaribu kuchezesha titi kama linacheza vizuri (free or movable at the base) hapo utakuwa upo vizuri. Pia kama hakuna aina yoyote ta uvimbe alio ubaini.

Endapo utagundua kuna ugumu wowote kwenye titi ambayo ni kiashiria cha uvimbe au titi kutotembea kwenye kitako chake basi ugundue ni dalili mbaya.

Njia ya pili: Kaa kwenye kiti au kitanda kisha nyanyua mikono juu kisha mwambie rafiki yako akuchunguze, vitu hatarishi ni hivi:

  • Uwepo wa mbonyeo kwenye titi
  • Chuchu kuingia ndani (nipple retraction)

Hizo ni dalili mbaya kwa mchunguzi atakapo toa taarifa, na inafaa uende hospitali ili kuchukua vipimo vya maabara haraka.

Vipimo Hospitali ili Kugundua Uwepo wa Saratani ya Matiti.

Kugundua kama dalili unazopata zinasababishwa na saratani ya titi daktari atapendekeza ufanyiwe uchunguzi unaojumuisha

  • Utrasound: ultrasound husaidia kupata picha ya sehemu ya ndani ya titi. Ultrasound hutumia mawimbi ya sauti kutengeneza picha hizi.utrasound inamsaidia daktari kutofautisha kati ya uvimbe usio saratani (benign cyst) na uvimbe ambao ni saratani (malignant tumor)
  • Breast biopsy: kipimo hichi kinajumuisha kuchukuliwa kwa kiasi kidogo cha nyama ya titi na kupelekwa maabara ili kufanyiwa vipimo

Mikakati ya kimaisha ili kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.

  1. Pata Vitamin D ya kutosha: Vitamin D inahusika katika kila seli ya mwili wako na ni moja ya Vitamn muhimu inayopatikana kiurahisi itakayokusaidia kuzuia kupata saratani. Vitamin D inafanya kazi ya kuua seli ambazo ni za muda mrefu na zisizohitajika (aptosis) ili kusaidia ukuaji wa seli mpya. Kwa hivo seli za saratani pia huweza kufa katika mtiririko huu. Vitamin D hutengenezwa  pale unaporuuhu mwili kukaa juani, hivo hakikisha unapata mwanga wa jua wa kutosha kila siku.
  2. Weka ratiba ya kufanya mazoezi: mazoezi husaidia kuweka sawa uzito, sukari yako na kuimarisha ufanyaji kazi wa homoni ya insulin
  3. Tumia virutubisho vya omega 3 mara kwa mara:. Upungufu wa omega 3 kwenye mwili huongeza hatari ya kupata saratani ya titi.
  4. Tumia kiungo cha turmeric(manjano) kwa wingi: kama unataka kuzuia saratani yoyote basi hutakiwi kukosa kiungo hiki nyumbani kwako.
  5. Usitumie pombe: ama punguza kwa kiasi kikubwa.
  6. Mama anatakiwa kunyonyesha mtoto kwa miezi sita bila kuacha. Tafiti zinasema kwamba inaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya titi.

Jaribu Cancer Care Package yetu:

Cancer care package kutoka kwetu ina virutubisho na dawa asili aina tatu zilizofanyiwa utafiti na kuhifadhiwa kwenye mfumo wa vidonge ambazo zitakusaidia

  • Kuimarisha kinga ya mwili na hivo kuzuia kutokea kwa saratani
  • Kupunguza madhara na dalili mbaya kama kutapika, maumivu, na uchovu kunakotokana na tiba ya Chemotherapy na Radiotherapy.
  • Kusaidia kutibu saratani pale ambapo virutubisho hivi vitatumika pamoja na dawa za hospitali
  • Kuzuia ukuaji wa seli za saratani na kusaidia uponaji haraka wa vidonda na
  • Kuongeza uzalishaji wa seli nyeupe za damu kwenye mwili ambazo hupambana na seli za saratani.

Unaweza kupata virutubisho hivi kwa kutembelea stoo yetu, bonyeza hapa.

Umegundulika na Saratani ya Matiti? nini cha Kufanya

Pale inapotokea tayari umegundulika kwamba una saratani hatua ya kwanza hakikisha unapata vipimo zaidi hata mara 4 sehemu tofauti tofauti. Hii ni kutokana na kesi nyingi zinazotokea pale ambapo unapimwa na kuonekana una saratani lakini ukirudia kupima huna saratani.

Kabla hujachukua uamuzi wa kuanza tiba ya mionzi na kemikali (radiotherapy na chemotherapy) na kabla hujaamua kufanyiwa upasuaji kuondoa titi lako, hakikisha vipimo vyako vimerudiwa mara kwa mara ili kujiridhisha kwamba kweli una saratani. Kwa hiyo usipoteze matumaini saratani ikiwahi kugundulika hupona mapema.

Share and Enjoy !

Shares
Shares