Tatizo la tumbo kujaa gesi imekuwa kubwa kwa siku za hivi karibuni. Hii inatokana nalishe mbovu tunayokula kila siku kwa kutegemea zaidi vyakula vya haraka na bei rahisi (fast foods & snacks). Vyanzo vingine vya tatizo ni msongo wa mawazo, matumizi ya vidonge mara kwa mara na mazingira yenye sumu yanayotuzunguka kama moshi wa magari na kemikali za viwandani.
Tunafahamu jinsi inavoleta usumbufu kwa tumbo kujaa gesi. Kila mara utahitaji kwenda chooni kujisaidia na kujamba. Licha ya usumbufu huu ,tatizo la tumbo kujaa gesi inaweza kuwa ni kiashiria cha matatizo makubwa ya kiafya. Mfano fangasi kwenye mfumo wa chakula. Fangasi hawa husababisha upate alegi ya vyakula mbalimbali, magonjwa ya autoimmune na hata saratani ya tumbo.
Dalili za Tumbo Kujaa Gesi
Kuwa na gesi tumboni ni tofauti kabisa na kitambi. Kitambi kinaweza kuwa cha muda mrefu lakini tumbo la gesi ni la muda tu baadae husinyaa na kurudi katika hali ya kawaida kwani huletekezwa na hewa kukwama tumboni na kufanya tumbo kutanuka. Kwa watu wengine tumbo linaweza kuwa kubwa kama mjamzito.
Kwa bahati nzuri ni kwamba tatizo la gesi tumboni unaweza kulitatua ukiwa nyumbani kwako kwa kurekebisha tu mpangilio wa lishe yako. Kwa kesi chache mfano kama tatizo linakutokea mara kwa mara basi kuna haja ya kupanga appointment ukaonana na dactari kwa vipimo. Dalili zingine zinazoambatana na tumbo kujaa gesi ni kama
- Homa
- Muwasho kwenye koo, machozi
- Kukosa choo au kupata choo kigumu na kuharisha
- Uwepo wa damu kwenye hajakubwa au mkojo
- Kupungua kwa uzito kusiko kawaida
- Maumivu kwenye sehemu za tezi hasa kwenye koo na kwapa
- Mwili kukosa nguvu na uchovu sana
- Kuvurugika kwa hedhi
- Bawasiri
- Ubongo kutofanya kazi vizuri
Nini Husababisha Tumbo Kujaa Gesi?
Unaweza ukawa unajiuliza ni kitu gani hasa ambacho ni chanzo cha tumbo kujaa na kufutuka kana kwamba umeshiba sana. Kuna vitu vingi nyuma ya pazia vivoletekeza tumbo kujaa. Kuanzia kwenye aleji, kuvurugika kwa homoni, matatizo kwenye tezi ya thairodi, shida kwenye mfumo wa chakula, na mengine mengi.
Inaweza kuwa ngumu kujua kinacholetekeza tumbo kujaa geni kwa upande wako lakini kadiri unavojifunza zaidi na kuusoma mwili wako basi utajua vitu gani vya kuepuka.Huwa nasema kila siku kwamba daktari wa kwanza wa mwili wako ni wewe mwenyewe. Ni muhimu kufatilia kwa ukaribu mabadiliko ya mwili wako.
Sababu 8 Zinazoletekeza Tumbo Kujaa Gesi
Matatizo kwenye Mmeng’enyo wa Chakula
Magojwa kama Ulcerative colitis, celiac disease na IBS-inflammatory bowel syndrome huletekeza kujaa gesi kwa tumbo
Maji kubakizwa mwilini (fluid retention)
Wakati fulani maji yanaweza kuabakizwa kwenye sehemu fulani za mwili kama kweye magoti, tumboni na kwenye nyonga. Maji haya huletekeza maumivu makali kwenye joints na tumboni. Uwepo wa maji tumboni hujulikana kama ascites na inaweza kuashiria kwamba una tatizo kwenye ini au maambukizi ya bacteria.
Ndio maana kuna umuhimu wa kufanya vipimo kama una homa ya ini (hepatitis B). kama kuna shida ya ini basi utapata dalili zingine kama kichfuchefu, macho na ngozi kuwa njano, kupungua uzito, kutapikadamu na chakula kutosagwa tumboni.
Mwili kukosa maji (Dehydration)
Umewahi kufuatilia siku ukiwa umekunywa sana pombe ama kula zaidi vyakula vyenye chumvi kwa wingi na tumbo likajaa gesi?. Mwili unapokosa maji hufanya uchakataji na usagaji wa chakula kuwa mgumu. Mwili unapokosa maji ya kutosha hufanya kazi ya kuvuta na kuhifadhi maji mengi zaidi pale utakapokunywa maji ili kuepuka kutokea kwa upungufu huu. Maji yanapokuwa mengi kupita kiasi ndipo sasa unaweza kupata choo kigumu ama kukosa choo. Hakikisha unakunywa maji mara nyingi zaidi kila siku ili kuepuka tumbo kujaa gesi.
Kukosa choo ama kupata choo kigmu/Constipaton
Constipation inaweza kuwa sababu kubwa ya kwanini tumbo lijae gesi. Constipation inaweza kusababisha choo kigumu, maumivu tumboni na kukosa choo kwa muda mrefu. Kukosa choo na choo kigumu husabishwa na ulaji wa vyakula vilivyokobolewa sana visivyo na kambakamba, matumizi kidogo ya maji, msongo wa mawazo na kuishi bila kufanya mazoezi.
Alegi ya Chakula
Alegi ya vyakula mbalimbali kama maziwa, mayai na ngano vinaweza kuwa ni sababu ya kujaa gesi kwa tumbo lako. Kuna aina nyingi ya vyakula inaweza kusababisha upate mzip ama alegi. Cha kufanya sikiliza mwili wako unasemaje pale unapokula chakula. Kama mwili unakataa aina fulani ya vyakula na unapata mcharuko kama kuvimba, kuharisha, ama kutapika basi usitumie chakula hicho.
Maambukizi
Kama mwili unapambana na maambukizi aidha ya bacteria, virusi, fangasi au vimelea wengine basi utapata tatizo la kujaa gesi tumboni kutokana na mpambano wa ugonjwa na seli nyeupe za damu.
Majeraha Kwenye Mfumo wa Chakula
Wakati mwingine unaweza kupata gesi tumboni kutokana na vidonda ama uvimbe kwenye baadhi ya sehemu za mfumo wa chakula kama utumbo mdogo na utumbo mpana. Uvimbe unaweza kuzuia utolewaji wa uchafu na kuletekeza gesi na maji kukwama.
Mabadiliko ya Homoni
PMS (pre menstrual syndrome) ikimaanisha mkusanyiko wa dalili zisizo za kawaida za kipindi cha hedhi ni chanzo cha tumbo kujaa gesi. Tatizo linaweza kuwa kubwa kama una uvimbe kwenye kizazi na hedhi yako inavurugika. Kwanini wanawake hupata gesi tumbo wakati au karibia na kipindi cha hedhi? Mwanamke anapokaribia hedhi kiwango cha homoni ya estrogen huongezeka na ukuta wa mfuko wa mimba kuongezeka. Pale anapopata siku zake basi damu na maji mengi hutolewa nje na hivo tumbo kurudi katika hali ya kawaida.
Saratani
Moja ya dalili za saratani ya utumbo mpana na saratani ya mfuko wa mimba ni tumbo kujaa gesi. Ndio maana ni muhimu kuongea na daktari wako pale ambapo umejaribu kila njia ya kundoa tatizo lako lakini bado halijaisha.
Vyakula vya Kuepuka pale Unapotaka Kutibu Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi
- Vyakula vya sukari na snacks zilizooongezewa utamu
- Nafaka na vyakula vya nafaka hasa ngano na Maharage huongeza uzalishaji wa gesi tumboni
- Vinywaji vilivosindikwa kama soda (Carbonated drinks)
Njia zingine za Kukusaidia Kuondokana na Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi
- Tembelea hospitali mara kwa mara kuonana na daktari
Kutokana na kwamba tumbo kujaa gesi inaweza kuletekezwa na matatizo mengine mengi ya kiafya kama tulivosoma pale juu kuna umuhimu kufanya vipimo mara kwa mara ili kujua chanzo cha tatizo lako. Kumbuka hakuna kipimo kimoja cha kujua kinachokusumbua ni vyema kuongea na dactari wako ili akupe ushauri na vipimo stahili. - Weka ratiba ya kufanya mazoezi: Kufanya mazoezi itakusaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa mfumo wa chakula, kurahisisha usafirishaji, na hivo kutoa sumu mwilini. Fanya mazoezi walau dakika 30 mpaka 60 kwa siku mara 3 kwa week.
- Kunywa maji ya kutosha: Maji hurahisisha usagaji wa chakula na utolewaji wa choo, Hakikisha unakunywa maji kila unapopata kiu. Hakuna kipimo maalumu cha kiwango cha maji unachotakiwa kutumia unaweza kuanza na glass 6 mpaka 8 itategemea na shughuli unazofanya na mazingira unayoishi.
- Punguza msongo wa mawazo
Tiba Kupitia Ya gesi Kupitia vidonge asili vya kayam
Vidonge hivi asili vimekuwa yakitumika kwa muda mrefu huko india kwa ajili ya changamoto mbalimbali kama kiungulia, gesi tumboni , maumivu ya kichwa, na kukosa choo.
Hivi sasa vidonge hivi yameonekana kutibu magonjwa mengine zaidi kama bawasili, kuharisha na kuimarisha usagaji wa chakula tumboni.
Namna ya kutumia Kayam kutibu gesi tumboni
Meza vidonge viwili vya Kayam, usiku kabla ya kulala. Meza kwa wiki mbili.