Ongeza ufanisi katika tendo la ndoa

Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu na nguvu za kiume na jinsi ya kuimarisha uwezo wa tendo la ndoa. Kama unaswali maoni ama unahitaji kufika ofsini kwetu endelea kutuandikia kwa namba yetu iliyopo chini ya makala hii.

Testosterone ni nini?

testosterone na uwezo wa tendo la ndoa

Testosterone ni homoni muhimu katika afya ya mwanaume. Husaidia kurekebisha mood, kuongeza kumbukumbu, uwezo wa kufikiri , kuimarisha ufanisi kwenye tendo la ndoa na misuli na mifupa mwilini..

Upungufu wa kichocheo hiki huleta madhara makubwa ikiwemo kupungua kwa misuli ya mwili, kushuka uwezo wa kufanya tendo na kuongezeka kwa uzito na kitambi.

Umri na Kiwango Cha Testosterone

Kichocheo cha testosterone ambacho hupatikana zaidi kwa upande wa mwanaume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanaume. Kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testosterone kinapungua.

Kupungua kwa kichocheo hiki inaanza baada ya miaka 30 kwa wanaume. Kuungua huku  kunaambatana na kuvimba kwa tezi dume (prostate gland), kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume.

Virutubisho gani vinahitajika kuzalisha homoni ya testosterone.

Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali. Baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya zinc na vitamin D3. Vitamin D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi

Wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jioni karibia na kuzama ni muda mzuri wa mwili kujitengenezea vitamin D. Utakubaliana na mimi kuwa wengi wetu tunakosa vitamini D kwa sababu muda mwingi tunautumia tukiwa ndani tukiendelea na shughuli zetu. Zinc ni madini muhimu ambayo hupatikana kwenye baadhi ya vyakula kama karanga, mbegu za maboga, mayai na maziwa.

Nini hasa kinasababisha kupungua kwa kichocheo cha testosterone.

Baada  ya kuangalia kichocheo kikuu cha testosterone hebu tujifunze kwa undani kuhusu homoni ama vichocheo vingine ambavyo vina mchango katika afya ya unyumba au tendo la ndoa

Insulini na tendo la ndoa

Najua umeskia kuwa insulin inafanya kazi ya kurekebisha sukari yako kwenye mwili, ni kweli kabisa nakubaliana na hilo. Lakini pengine hujawahi kupata dondoo ni kwa kiasi gani homoni hii ina mchango mkubwa kwenye swala la sex. Hebu tutazame sasa ni kivipi ili upate ufahamu.

Pale sukari inapokuwa nyingi zaidi kwenye damu, kongosho humwaga insulin kwenye damu ili kurekebisha kiwango kile cha sukari. Sukari nyingi hubadilishwa na kuhifadhiwa kama mafuta kwenye seli za kuhifadhi mafuta mwilini.

Kadiri insulin inavomwagwa zaidi kwenye damu itafikia mahali mwili hausikii uwepo wa insulin kitaalamu tunaita Insulin resistence, na ndipo mtu ananza kuugua kisukari. Insulini inapokuwa nyingi kwenye damu basi utolewaji wa testosterone hushuka na ndio hupelekea mwanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.

Leptin na Tendo la Ndoa

Kazi ya homoni hii ni kuzuia au kukata hamu ya kula pale mwili unapokuwa umeshiba kwa kuamrisha ubongo wako. Sasa pale unapokula wanga na sukari nyingi zaidi hupelekea leptin kushindwa kufanya kazi ipasavyo yaani mwili hausikii uwepo wa leptin kitaalamu tunaita Leptin resistence.

Najua umekutana na mtu akikwambia anakula anashiba kisha baada ya muda mfupi anaanza kujiskia njaa tena. Ukiona hivi ujue huyu mtu ni mlevi wa sukari ndio maana imepelekea kupunguza ufanisi wa leptin.

Kama utazidi kujisikia njaa zaidi tafsiri yake utazidi kula zaidi sukari na wanga na ndivyo insulin itamwagwa zaidi kwenye damu kubadilisha sukari kuwa mafuta. Mafuta haya yatazidi kuhifadhiwa na kukufanya uendee kuwa mnene na kitambi. Hivo homoni hizi huenda mkono kwa mkono.

Growth Hormone

Homoni hii hutolewa na tezi ya pituitary mara nyingi  mtu akiwa amelala. Kazi yake kubwa ikiwa ni  kuongeza ukuaji wa misuli, kusaidia mwili kuchoma mafuta, na pia kuongeza hamu ya tendo la ndoa. Hivo kupungua kwa homoni hii hupelekea uzito kuendelea kuongezeka, kupungua kwa misuli ya mwili na pia kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.

Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya kupungua kwa uzalishaji wa kichocheo hiki cha ukuaji(Growth hormone) na kupungua kwa uzalishaji wa testosterone na hivo kupelekea kushuka kwa ufanisi kwenye tendo la ndoa.

Homoni ya cortisol na Tendo la Ndoa

Pale unapokuwa na msongo wa mawazo basi mwili kupitia tezi ya Adrenali hutoa homoni ya cortisol ili kupambana na hali hiyo. Lakini tafiti zinasema kwamba kadiri mwili unavozalisha na kumwaga costisol nyingi zaidi basi inapelekea mwili kutohisi uwepo wa homoni ya leptin. Homoni ambayo tumeona kuwa inakutaarifu kuwa umeshiba.

Hebu unganisha haya mtukio. Cortisol imeongezeka, mwili hauhisi leptin manake utazidi kuwa mlevi wa wanga na sukari, kisha insulini itamwagwa zaidi naa zaidi ili ipunguze sukari iliyozidi. Utazidi kuwa mnene kutokana na sukari iliyozidi kwenye damu kubadlishwa kuwa mafuta.

Uzalishaji wa homoni ya testosterone utashuka na mwishowe ufanisi wa tendo la ndoa unashuka na unakuwa muhanga wa nguvu za kiume. Kwa wanawake wanakuwa wahanga wa matatizo ya hedhi na uvimbe kwenye ovary.

Aina za vyakula na virutubisho vinavyosaidia kuongeza uzalishaji wa kichocheo cha testosterone.

Ijapokuwa kuna njia nyingi za kusaidia kuongeza kiwango cha kichocheo cha kiume au Testosterone. Uzalishaji wa kichocheo hii unategemea zaidi upatikanaji wa viini lishe fulani ambavyo vinapatikana ndani ya vyakula tunavyotumia

1.Madini ya zinc

Zinc ni muhimu zaidi katika uzalishaji wa homoni ya testosterone. Inakadiriwa kuwa 45% ya watu wazima wana upungufu wamadini ya zinc kutokana na matumizi madogo ya vyakula vyenye madini haya. Baadhi ya vyakula ambavyo madini haya hupatikana ni mbegu za maboga, maziwa, maharage, na vyakula vyenye protein kwa wingi kama nyama na samaki

2.Kokomanga

Tunda hili zuri lenye rangi nyekundu likiwa limeiva limekuwa likitumika kama dawa kwa karne nyingi sasa. Kutokana na uwezo wake mkubwa kama kiondoa sumu (antioxidant), pia upatikanaji wa vitamini A,C, E na madini ya chuma.

Tafiti za kisayansi zinasema kuwa unywaji wa glass 1 ya juisi kwa siku itokanayo na matunda haya inaongeza kwa asilimia 16 mpaka 30 ya hamasa ya tendo la ndoa. Lakini pia inashauriwa zaidi kula tunda lenyewe ili kwanza kufaidi nyuzinyuzi (fiber) ambazo zina umuhimu kiafya pia itakusaidia kutokula kiwango kikubwa cha sukari kilichopo kwenye matunda.

3.Mafuta ya mizeituni

Mafuta ya mizeituni yana uwezo mkubwa sana wa kuongeza kiwango cha kichocheo cha testesterone kinachozalishwa na mwili. Tafiti zinasema watu wanaotumia mafuta ya mizeituni kila siku,kiwango cha testosterone huongezeka kwa asilimia 17 mpaka 19 ndani ya week.

4.Nazi

Mwili unahitaji mafuta mazuri ili kutengeneza vichocheo ikiwemo kichocheo cha testosterone. Nazi na aina zingine za nuts kama karanga zinasaidia mwili kutengeneza mafuta mazuri ambayo yanahitajika na mwili. Pia mafuta yanayopatikana kwenye nazi husaidia mwili kuwa na uzito mzuri na pia kupunguza mafuta mabaya yasiyohitajika na mwilini.

Hapo utagundua kuwa kurekebishwa kwa uzito wa mwili basi kunasaidia uzalishaji wa kichocheo cha kiume. Pia utakubaliana nami kuwa uzito mkubwa ni chanzo cha tatzo la upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa kichocheo cha kiume.

5.Mboga za Majani

Mboga za broccoli na cauliflower zinasaidia mwili wa binadamu kutoa kiwango cha kichocheo cha estrogen kilichozidi ndani ya mwili na hivyo kuongeza kiwango cha testosterone ndani ya seli

6.Protini itokanayo na Maziwa

Protini hii ambayo hupatikana kwenye sehemu ya maji ya maziwa inazuia mwili kutengeneza kiasi kikubwa cha kichocheo cha cortisol. Na hivyo kuongeza uzalishwaji  na ufanyaji kazi wa wa kichocheo cha  testosterone. Hapa ieleweke kwamba homoni hizi mbili huwa zinapishana moja ikiwa nyingi kwenye damu basi ingine huwepo kwa kias kidogo kwenye damu.

Dalili zifuatazo zinaonesha kwamba una upungufu wa kiwango cha testosterone

Njia zingine za kukusaidia Kumarisha uwezo wa Tendo la Ndoa

1.Mazoezi ya mwili

Kupunguza uzito usiohitajika kwa kufanya mazoezi ya  mwili ni njia mojawapo asilia ya kuongeza kiwango cha testosterone.Mazoezi pia husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kuelekea kweye uume.

2.Punguza msongo wa Mawazo

Mwili unapokuwa na msongo wa mawazo basi hupelekea uzalishaji kwa wingi wa homoni iitwayo cortsol ili kupamban na hali hiyo. Lakini upande wa pili ni kwamba kiwango kikubwa cha cortsol kwenye damu hupelekea ufanyaji kazi ya homoni ya kiume yaani testosterone kupungua

3.Punguza matumizi makubwa ya Wanga na Sukari

Matumizi makubwa ya vyakula vyenye wanga na sukari hupelekea mwili kutengezeza kiwango kikubwa cha homoni ya insuini ili kubadilisha kiwango hcho cha sukari na kukihifadhi kama mafuta. Mpenzi msomaji tambua kwamba kadiri unakula wanga na sukari nyingi ndipo kiasi kikubwa cha insulini kinavomwagwa kwenye damu na ndivyo ufanini na utolewaji wa homoni ya kiume unavopungua.

Tezi dume ni nini

Hii ni tezi (kokwa) ambayo inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kutengeneza maji maji ya uzazi kwa mwanaume(shahawa) ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizotengenezwa kutoka kwenye korodani.

Shahawa pia husaidia kusafirisha mbegu za kiume na kuzifanya zibaki hai kwa muda unaostahili. Hakikisha unasoma makala ya tatizo hili la tezi dume ambayo tumeiandika kwa kirefu na kuchambua kwa kina. Bofya hapa kusoma kuhusu kuvimba kwa tezi dume na athari kwenye tendo la ndoa.

Hitimisho

Mpenzi msomaji baada ya kuona kuwa testerone ndio kichocheo kinachomfanya mtu awe mwanaume. Yaani kuweza kufanya majukumu ya kimwili kama mwanamme. Utakubaliana nami kwamba  upungufu wa kichocheo hiki moja kwa moja kunapelekea upungufu wa nguvu za kiume. Tatizo ambalo linasumbua watu wengi sana kwa sasa.

Nguvu za kiume imekuwa topic kubwa sana kwa sasa, wataalamu wengi wamekuwa wakiongelea jambo hili kwa jinsi wanavolifahamu. Lakini kwa bahati mbaya wengi hawagusi chanzo kikubwa cha tatizo hili ambacho ni mfumo wa homoni. Pamoja na kwamba kuna sababu zingine kama vyakula na vinywaji lakini kuvurugika kwa homoni ni chanzo kikuwa ambacho kinaletekeza matatizo kama kushuka kwa hamu ya tendo la ndoa, kuwahi kufika kileleni na jogoo kushindwa kuwika.

JARIBU KUTUMIA MALE SEX DRIVE PACKAGE YETU kwa gharama ya sh 150,000/= tu

Ni muunganiko wa dawa mbili za zinc na confido, zitakusaidia

  • Kuimarisha uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kuchelewa mpaka dakika 20 bila kuchoka
  • Kuongeza uzalishaji wa mbegu(sperm count) na ubora wa mbegu(sperm quality)
  • Kuimarisha mzunguko wa damu kuelekea kweye uume na hivo kukufanya usichoke mapema unapofanya ngono
  • Inafaa kwa wanaume wote wanaowahi kufika kileleni, kukosa hamu ya tendo la ndoa na wanaoshindwa kuwapa mimba wanawake.

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata tiba kwa Tsh 150,000/=

Share and Enjoy !

Shares
Shares