Mwongozo wa hedhi salama

Hedhi salama ni ipi

mzunguko wa hedhi

Kwa mwanamke kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi ni jambo la kujivunia na linaloleta heshima sana. Mzunguko wa hedhi unaweza kutoa picha kamili nini kinaendelea kwenye mwili wa mwanamke. Kama mfuko wa mimba unapata mzunguko mzuri wa damu, homoni zako zinbalansi, au kama mayai yanatolewa kwenye ovari.

Katika makala yetu ya leo tutaangali hatua za mzunguko wa hedhi, jinsi ya kutumia viashiria ya hedhi ili kujua afya yako na jinsi ya kutumia tiba asili (natural therapies) kama fertility cleansing, tiba za mimea, ama lishe katika kuweka mzunguko wenye afya.

Hedhi ni kitu gani?

Hedhi ni muunganiko wa yai ambalo halikurutubishwa pamoja na damu inayotokana na kumomonyoka kwa tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba (uterus). Kitendo hiki hutokea kila mwezi kwa mwanamke.

Jinsi mwili unafofanya kazi mpaka kupatikana kwa hedhi

Kupata hedhi ni kitendo kinachoratibiwa na mzunguko wa homoni. Kwa maelezo mafupi na rahisi ni kwamba inaanza na eneo la ubongo linaloitwa hypothalamus kuzalisha homoni ya gonatrophin (GnRH) ambazo zinachochea tezi ya pituitary kuzalisha homoni ya luteinizing(LH) na Follicle stimulating hormone(FSH).

Homoni hizi mbili yaani LH na FSH hulenga kuamrisha ovari kuzalisha homoni za estrogen na progesterone. Ovari napenda kuita ni kiwanda cha kuzalisha na kuhifadhi mayai. Fikiria homoni hizi zinafanya kazi kama vile mfano wa vitabu vilivyopangwa mezani kwa wima vikilaliana, ikitokea kitabu cha mwanzo kimeondolewa kwenye mstari basi vyote vinaanguka.

Ni mlolongo mrefu na kama ikitokea mvurugiko wa homoni moja basi mtiririko wote unaharibika na unaanza kukosa hedhi au hedhi kuvurugika, na matatizo mengine mengi ya uzazi ikiwemo uvimbe na ugumba. Zifuatazo ni hatua za mzunguko wa hedhi.

Hatua za Mzunguko wa hedhi

Follicular phase

Sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus hutambua kiwango cha estrogen na progesterone ambacho huzalishwa na ovari. Kama kichocheo cha estrogen kikipungua ndani ya mzunguko wa hedhi basi ubongo hutoa GnRH ambayo huamrisha pituitari kuzalisha FSH . FSH inachochea kuanza kukua kwa mayai kuanzia 10 mpaka 20.

Kati ya haya ni yai moja pekee ambalo hukomaa na kuwa tayari kurutubishwa ndani ya mwezi husika. Kadiri mayai madogo yanavokuwa huzalisha homoni ye estrogen ambayo kazi yake ni kuimarisha na kuundaa ukuta wa uterus ili kupokea kiumbe baada ya urutubishaji kufanyika.

Kadiri kiwango cha estrogen kinavyopanda ndivyo mwanamke ataanza kupata ute mzito wa rangi ya maziwa. Kuongezeka kwa kiwango cha estrogen huchochea utolewaji wa GnRH kutoka kwenye ubongo ambayo huchochea FSH na LH kwa wingi. Homoni hizi mbili huchangia utolewaji wa yai kwenye kikonyo chake kitendo hiki huitwa ovulation. Baada ya ovulation kiwango cha FS na LH huanza kupungua taratibu.

Luteal phase

Kutolewa kwa yai inafuatiwa na hatua hii ya luteal phase. Kabla ya kuendelea nataka ufahamu baadhi ya misamiati: Kumbuka baada ya yai kutolewa kwenye kikonyo linabaki kovu kama shimo. Kovu hili huitwa corpus luteum. Kazi yake ni kuendelea kuzalisha progesterone na kiwango kidogo cha estrogen.

Ukuta wa juu mwembamba wa uterus ambao humomonyoka tunauita endometrium. Kwahivo baada ya yai kutolewa progesterone inasaidia kuendelea kuurutubisha ukuta(endometrium) ili uweze kupokea kiumbe.
Endapo hapatawepo na mbegu ya kiume(sperm) kurutubisha yai basi ukuta wa endometrium huanza kubomoka na kutolewa nje kama hedhi.

Jinsi ya Kuhesabu Siku za Mzunguko wa Hedhi

Siku ya kwanza ya mzunguko ni siku ambayo unapata hedhi katika mwezi husika. Siku zote kati kuanzia siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya ovulation (yai kutolewa) huitwa follicular phase. Kipindi hiki kikawaida huchukua siku 14 lakini hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.

Luteal phase ni kipindi kati ya ovulation(siku ambapo yai limetolewa) na siku ya kwanza kupata hedhi katika mwezi,ni katika kipindi hiki ambapo yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye ukuta wa uterus. Kama kipindi (luteal phase) kitakuwa kifupi sana chini ya siku 12 basi itakuwa ngumu kwa kiumbe kujishikiza kwenye ukuta.

Hedhi ya Kawaida ni ipi

Najua wanawake wengi mtakuwa mnajiuliza ni mzunguko gani wa hedhi ambao ni wa kawaida kwa mwanamke kuwa nao. Ukweli ni kwamba hakuna jibu la mojakwamoja kwamba mzunguko ule ni wa kawaida kutokana na kwamba miili imetofautiana.

Lakini taarifa muhimu za kujua kama mzunguko wako ni mzuri ni kujua jumla ya siku za mzunguko wako, kiwango cha maumivu wakati wa hedhi, rangi na kiwango cha bleed yako. Taarifa hizi zinaweza kukusaidia kujua ni aina gani ya lishe au tiba asilia utumie ili kurekebisha na kubalansi hedhi yako.

Urefu wa Mzunguko wa Hedhi

Mzunguko wa kawaida unatakiwa kuchukua siku 21 mpaka 35. Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na mzunguko mfupi zaidi au mrefu kuliko huu. Kiwango cha homoni na utolewaji wa yai ndivyo vinatengeneza uwiano wa mzunguko wa hedhi. Kama yai halitatolewa itapelekea kuvurugika kwa hedhi na tena kupelekea yai kutotolewa, inakuwa ni kitu endelevu. Kuna vihatarishi vingi vinavyoweza kuvuruga homoni za kike kimojawapo ikiwa ni msongo wa mawazo.

Jinsi ya kutumia Viashiria vya Hedhi ili Kutambua Uwiano wa Homoni Zako.

Hapa chini nimeelezea uhusiano kati ya viashiria hivi na homoni zako. Lengo langu ni kukuonesha namna ya kuusoma mwili na kuusikiliza pale unapoeda nje ya mstari. Mzunguko wa hedhi ni njia muhimu ya kuusoma mwili kuhusu uwezo wa kushika mimba.

Kukosa hedhi

Kukosa hedhi mara moja inaweza isiwe tatizo. Mpangilio wa homoni ni kitu sensitive sana na kinaweza kuathiriwa tu na msongo wa mawazo. Lakini kwa kiasi kikubwa unaweza kujirekebisha wenyewe. Kukosa hedhi pekee siyo kiashiria kwamba hutaweza kushika mimba. Maana yake yawezekana mayai yanatolewa(ovulation) lakini usipate hedhi. Kukosa hedhi kwa zaidi ya miezi 6 huitwa Amenorrhea na inaashiria kuna tatizo ambalo unahitaji kumwona daktari haraka.

Period fupi

Mzunguko mfupi unaweza kuleta matatizo kwenye uwezo wa kushika mimba. Baadhi ya vihatarishi ambavyo hufupisha mzunguko wako ni kama kukosa ovulation, upungufu wa virutubisho mwilini, uzito mdogo sana, upungufu wa damu .

Period ndefu

Mzunguko mrefu wa hedhi unaweza kuashiria kuvurugika kwa homoni na mayai kutopevuka. Homoni ya progesterone ambayo hutolewa na mwili husaidia kuzuia bleed kuemdelea. Kama estrogen ni nyingi na progesterone ni kidogo bleed inaweza kuendelea kwa siku nyingi zaidi kuliko kawaida

Hedhi nzito na nyingi zaidi

Kupata hedhi nzito na nyingi kupita kiasi husababishwa na ukuta wa uterus kusisimka zaidi. Msisimko huu hutokana na wingi wa estrogen, inapelekea ukuta kumomonyoka kupita kiasi. Tatizo hili linaweza kurekebishwa kwa kurekebisha lishe yako na kutumia tiba ya mimea kwa ajili ya kurekebisha homoni. Upungufu wa vitamin A na C inaelezwa kuchangia bleed nzito. unaweza kutumia virutubisho kama multivitamin.

Hedhi kidogo inayoambatana na maumivu makali ya tumbo

Kama unapata hedhi nyepesi, nyekundu inaweza kuashiria kwamba mzunguko kwenye mfuko wa mimba ni mdogo. Unaweza kupunguza hali hii kwa kufanya masaji kwenye eneo la tumbo ukitumia mafuta ya mnyonyo, ama kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya moto.

Hedhi ya damu nyekundu inayong’aa

Kama hedhi inatoka ni damu mbichi na nyekundu ya kung’aa. inaonesha inatoka moja kwa moja kwenye kizazi. Na inaweza kuashiria jeraha kwenye kizazi au pengine mimba kuharibika. Ukipata hedhi au damu ya namna hii, jitahidi kuwahi hospitali mapema hasa kama ulipitisha hedhi, maana yawezekana ulishika mimba na imetoka.

Hedhi nzito yenye weusi ama brown

Hii inaonesha kwamba kuna masalia ya damu ya zamani kwa hedhi iliyopita. Kubaki kwa damu husababishwa na flow ya polepole sana na mzunguko mdogo ndani ya mfuko wa mimba. Unaweza kurekebisha tatizo hili kwa kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha, kufanya masaji eneo la tumbo na pia unaweza kujaribu fertility cleansing package yetu.

Hedhi yenye damu mpauko na maji zaidi.

Kama unapata hedhi ya namna hii inaonesha kwamba damu yako kiujumla haina ubora na inakosa virutubishi muhimu. Kula lishe nzuri husaidia unaweza pia kutumia virutubishi vingine kama Multivitamin na Spiriluna kuimarisha damu yako.

Kuganda kwa damu ya hedhi

Kuganda kwa damu ya hedhi inaweza kuwa siyo jambo na kutisha ukilinganisha na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu. Lakini yatakiwa kuendelea kufatitilia hedhi yako pia. Kama kuganda kwa hedhi yako kunatokea mara chache hasa mwanzoni mwa period, ni mabonge madogo madogo, yenye rangi nyekundu inayong’aa basi ni salama.

Lakini kama unapata mabonge mabubwa na inakuwa mfululizo basi yahitaji kumwona dactari kupata ushauri. Unatakiwa kumwona dactari haraka kwani kupata damu nzito yenye mabongemabonge kama unahisi unaweza kuwa na ujauzito yaweza kuashiria kwamba mimba imeharbika. Tumia maji ya kutosha na kufanya masaji eneo la tumbo kwa kutumia mafuta ya nyonyo (castor) ili kupunguza tatizo hili.

Kupata bleed kwenye kipindi kisichokuwa na hedhi

Bleed katikati ya vipindi vya hedhi ni tatizo linasowachanganya sana wanawake. Yaweza kusababishwa na kuvurugika kwa mpangilio wa homoni (rejea maelezo yangu pale juu)yai kutotolewa kwenye kikonyo chake(ovulation). Uvimbe unaotokana na kukua kupita kiasi kwa tishu laini za ukuta wa uterus(endometriosis), matumizi ya dawa za kupanga uzazi, mazoezi magumu na lishe duni

Kukosa kabisa hedhi(Amenorrhea)

Inaweza kutatiza pale ambapo unashika ujauzito lakini hupati hedhi kabisa. Kuwa na mzunguko mzuri ni hatua ya kwanza katika kujua kwamba unaweza kushika ujauzito. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuchangia hedhi yako kuvurugika kama msongo wa mawazo, lishe duni, uzito mdogo sana, kutumia vidonge vya kuzuia mimba, kuvurugika kwa homoni, umri kwenda (kukaribia menopause) na matatizo mengine ya kiafya.

Hatua 4 za kufuata ili kuhakikisha kwamba unapata mzunguko mzuri wa hedhi.

Kusawazisha vichocheo/hormones

Kama nilivokwisha kueleza pale juu kuna mstari mwembamba sana kati ya hedhi kuwa sawa na kuvuruga kwa hedhi. Makosa kidogo tu yanaweza kupelekea kuharibu mpangilio wa vichocheo na hivo kuvuruga hedhi yako. Tumia virutubisho mbalimbali kama Soy power, chai ya Pine pollen na Multivitamin kweka sawa vichocheo vyako.

Kuimarisha uwezo wa ini.

Ini pamoja na kazi zingine hufanya kazi ya kuondoa homoni zilizozidi mwilini. Kama kuna kiwango kikubwa cha estrogen ini linaweza kuzidiwa na kuhitaji usaidizi. Hakikisha unatumia tiba nzuri za mimea na virutubishi asili kusafisha ini lako kila mwezi. Unaweza kujaribu bidhaa hizi za asili zikakusaidia kusafisha ini.

Lishe

Lishe inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuweka hedhi yako sawa. Ni muhimu kutumia virutubisho vya aina nyingi ikiwemo vitamins, madini, mafuta, vidondoa sumu(antioxidants). Vyakula hivi ni muhimu kutumia kwa wingi kwenye mlo wako wa kila siku. Hakikisha unapangilia ili kila siku upate virutubisho hivi vyote kwenye milo yako.

Hapa chini nimeelezea vyakula kwa kila aina vya virutubishi . Nimekupa uhuru wa kupangalia kila mlo. Siyo lazima kula vyakula hivi vyote kwa mara moja, lakini ni uhimu kupata virutubisho vyote kwa siku. Vyakula vingi vina vitamin na madini mengi uataona maelezo hapa chini.

  • Madini ya chuma: Vyanzo ni mboga za kijani, maini, mayai na mbegu za maboga(unaweza kutumia pia unga wake kutengeneza chai, ama kuchanganya na uji)
  • Vitamin C na B: Vyanzo hoho nyekundu, machnungwa, broccoli, cabbage, nyanya na cauliflower.
  • Omega 3: Vyanzo vyake samaki, walnuts, na chia seeds
  • Fibers au kambakamba : Vyanzo ni mboga za majani kwa wingi na vyakula visivyokobolewa.
  • Madini ya zinc: mbegu za maboga na nyama
  • Vitamin D: kwa kupata mwanga wa jua walau dak 15 mpaka 20 kila siku. asubuhi au jioni
  • Vitamin E: vyanzo vyake ni mafuta ya olive, spinach, parachichi na almonds
  • Folic acid: vyanzo vyake: maini, spinach na maharage.
  • Vyakula vyenye mafuta mazuri; Vyanzo ni mafuta ya nazi, olive, parachichi na karanga

Punguza Msongo wa Mawazo

Stress huleta matoeko hasi kwenye hedhi yako kama usipoweza kujifunza namna ya kudhibiti. Stress za kazi, familia, uchumi binafsi na mengine mengi huvuruga mpangilio wa homoni zako. Stress huongeza utolewaji ya homoni ya cortisol ambayo huzuia uzalishaji wa GnRH (rejea maelezo yake pale juu) . Na kisha kupelekea mayai kutotolewa kwenye kikonyo(ovulation). Stress kwa wanaume hupunguza uzalishaji wa mbegu za kiume na hamu ya tendo la ndoa kwa wote. Mazoezi husaidia kupunguza athari ya msongo wa mawazo.

Tumia Evecare kurekebisha hedhi yako

Evecare ni dawa asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ya Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili

Baada ya kutumia Evecare tegemea kupata matokeo haya

  • Hedhi kutoka vizuri kwa siku chache siyo zaidi ya siku 4 ama 5
  • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
  • Homoni kubalansi
  • Kupata hedhi nyepesi ya kawaida
  • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
  • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

Bei ya Evecare ni Tsh 75,000/= Tunapatikana Dar, Magomeni.

Angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge feki vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Chati na daktari kwa whatsapp 0678626254 kuanza tiba

Share and Enjoy !

Shares
Shares