Mkanda wa jeshi ni tatizo gani?
Mkanda wa jeshi ni ugonjwa wa ngozi unaombatana na maumivu makali, ugonjwa huu unawapata watu ambao waliwahi kuugua tetekuwanga kwa kipindi cha nyuma. Virusi wa ‘varicella zoster’ ndio chanzo cha ugonjwa wa mkanda wa jeshi na vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Unapougua tetekuwanga na baadae ukapona virusi hawa hujificha kwenye mishipa ya damu kwa miaka mingi. Pale kinga ya mwili inaposhuka sana ndipo virusi hawa hujitokeza na kusababishwa ugonjwa mwingine wa mkanda wa jeshi.
Mkanda wa jeshi huwa na dalili za maumivu makali ukilinganisha na tetekuwanga sababu ugonjwa huu unaathiri neva za kwenye ngozi na wakati mwingine kuwa na dalili kama za mafua ambazo huisha baada ya week chache.
Dalili kuu za mkanda wa jeshi
Zifuatazo ni dalili kubwa za mkanda wa jeshi
- Ukurutu unaouma ambao huonekana kama malengelenge yanayosambaa kwenye ngozi hasa ya kifua, tumbo, usoni, kwenye mgongo na kwenye miguu na mikono
- Malengelenge yanayojikusanya mahali pamoja ama yalio katika mstari unaoanzia chini ya tumbo upande mmoja kukatiza mpaka kweye bega.
- Ukurutu mwekundu unaojikusanya mahali pamoja
- Kupata muwasho na wakati mwingine hali ya kuchomachoma kama sindano
- Kupata maumivu kwenye Ngozi ambayo huisha pale lengelenge linapopotea
- Mabadiliko katika uzito wa mwili na kukosa hamu ya kula
- Maumivu ya kichwa, mwili kuishiwa nguvu mara kwa mara na homa
- Kupata shida kwenye kuona pale malengelenge yanapotokea karibu na macho.
Swali la kujiuliza je unaweza kuugua mkanda wa jeshi zaidi ya mara moja? Kundi kubwa la watu huugua mkanda wa jeshi mara moja tu katika maisha yote. Hii ni kutokana na kwamba mwili unatengeneza kinga imara zaidi baada ya kupona. Kundi dogo la watu 10% ndio huugua mkanda wa jeshi zaidi ya mara moja.
Hatua za ukuaji wa mkanda wa jeshi(shingles).
Ugonjwa mkanda wa jeshi unakua kwa hatua na inaweza kuchukua muda mrefu mpaka kuweza kugundua ugonjwa.
Hatua ya kwanza huitwa prodromal stage: Katika hatua hii baadhi ya dalili huanza kujitokeza taratibu. Dalili za awali kama homa na kuumwa kichwa hufanana na dalili za magonjwa mengine na hivo kufanya utambuaji hasa kwamba una mkanda wa jeshi kuwa vigumu. Dalili hizi unaweza kuchanganya na tatizo la mafua.
Wagonjwa wengi huanza kutambua uwepo wa mkanda wa jeshi baada ya kuona dalili kama malengelenge yenye muwasho na hali ya kuunguza kwenye ngozi. Malengelenge haya yenye wekundu hujitokeza hasa upande mmoja wa mwili inaweza kuwa kushoto ama kulia. Ni muhimu kwa mgonjwa kufika hospitali ili kupata vipimo juu ya tatizo kwa sababu malengelenge haya inaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa wa Herps.
Inachukua muda gani kwa dalili za mkanda wa jeshi kupotea?
Malengelenge ya mkanda wajeshi yanapofikia hatua ya kuiva hadi kuwa na rangi ya mawingu baada ya wiki kadhaa huweza kutoboka na kutoa maji na kuacha kovu. Maumivu yanaweza kuendelea kwa wiki kadhaa kutokana na kundelea kujijenga kwa neva za mwili zilizoathirika( kitendo hichi huitwa postherapetic neuralgia). Inaweza kuchukua mpaka wiki nne kwa dalili kuisha kabisa.
Ugumu ambao wagonjwa wengi hupata ni pale dalili za mkanda wa jeshi kuingiliana na shughuli za kawaida na kumfanya mgonjwa kupata ugumu kwenye kula, kuoga, kufanya kazi, kutembea na hata kuona vizuri.
Mazingira hatarishi yanayopelekea kuugua mkanda wa jeshi.
Mkanda wa jeshi hujitokeza baada ya virusi wanaosababisha tetekuwanga kujitokeza tena kwa mara ya pili baada ya kujificha kwenye mwili kwa mda mrefu. Unapougua tetekuwanga basi mojakwamoja unabeba virusi ndani yako. Ukishapona virusi hawa wanajificha kwenye mizizi ya neva zako.
Kwa maana hiyo huwezi kuugua tetekuwanga mara mbili bali virusi hao watakufanya uugue mkanda wa jeshi siku zinazokuja. Virusi wa Varicella zoster wanaweza kukaa kimya(dormant) miaka yote pasipo kujitokeza tena. Lakini pale kinga inaposhuka sana ndipo utaanza kuugua mkanda wa jeshi. Mazingira haya hatarishi yanayoongeza hatari ya kupata mkanda wa jeshi ni kama
- Umri mkubwa, hasa kuanzia miaka 60 na kuendelea. Watoto na vijana wanaweza pia kupata mkanda wa jeshi japo dalili zao zinakuwa siyo kali ikilinganishwa na wenye umri mkubwa.
- Wanawake hasa wenye umri mkubwa huugua zaidi mkanda wa jeshi ukilinganisha na wanaume.
- Watu waliowahi kuugua magonjwa yanayoathiri zaidi kinga ya mwili kama ukimwi, saratani, kansa ya damu na lympoma.
- Matumizi ya vidonge ambavyo huzorotesha kinga ya mwili
- Historia ya familia. Kama ndani ya familia kuna watu waliwahi kuugua mkanda wa jeshi basi utakuwa kwenye hatari zaidi ya kuuugua.
- Kama uliwahi kupata ajali au shida kwenye neva basi hatari ya kupata mkanda wa jeshi ni kubwa kwa sababu tatizo hili linakuwa kufuata neva.
- Mwisho kabisa jitahidi kucontrol msongo wa mawazo na kuimarisha afya mfumo wa chakula. Msongo wa mawazo kupita kiasi hupunguza kinga ya mwili na hivo kukuongezea hatari ya kupata mkanda wa jeshi.
Je mkanda wa jeshi huambukizwa?
Unaweza kujiuliza kukaa karibu na mwenye tatizo hili anaweza kukuambukiza?. Tumeona pale juu kwamba virusi wanaosababisha mkanda wa jeshi hujitokeza katika mazingira ya aina mbili. Maambukizi ya mwanzo kabisa ambayo husababisha tetekuwanga na athari ya pili itokanayo na virusi waliojificha ndani ya mwili ambayo huleta mkanda wa jeshi.
Kwa kusema hayo maana yake ni kwamba kama hukuwahi kuugua tetekuwanga basi huwezi kuambukizwa mkanda wa jeshi, hata ukigusana na mgonjwa.
Njia asili za kutibu mkanda wa jeshi
Habari njema ni kwamba kuna tiba nyingi zisizo gharama ambazo unaweza kutumia nyumbani kwako ukapunguza athari ya tatizo. Tiba hizi asili hulenga zaidi katika kuimarisha kinga ya mwili sababu mkanda wa jeshi husababishwa na virusi.
Vyakula vya kutumia ili kutibu dalili za mkanda wa jeshi
- Vyakula vyenye Vitamn B kwa wingi- ni muhimu kutumia vyakula vyenye Vitamin B kutoka kweye vyanzo mbalimbali kama mtindi, mayai na nyama ya kuku. Vitamin B husaidia kujenga neva zilizoharibika kutokana na mashambulizi ya virusi.
- Kunywa maji ya kutosha. Maji husaidia kuflush virusi wengi zaidi kwenye mifumo ya mwili. Jitahidi kunywa glass 6 mpaka 8 kwa siku.
- Kitunguu saumu; kina kiambata cha Allicin ambacho husaidia kuimarisha kinga ya mwili
- Vyakula vyenye vitamin C kwa wingi; machungwa na matunda mengine ya njano yana vitamin C kwa wingi yatasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kuharakisha kupona.
- Mbogamboga za kijani- mboga hizi zina kiwango kikubwa cha beta-carotene na madini ya Calcium ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
- Asali: tafiti zinasema kwamba matumizi asali husaidia kupambana na virusi vya Varicella Zoster na hivo kutibu dalili za Mkanda wa jeshi. Chukua kiasi kidogo pakaa kwenye eneo lililoathirika mara mbili au tatu kwa siku.
Kwa upande mwingine vyakula vya kuepuka ili kupona mapema ni pamoja na
- Vyakula vya sukari- hupunguza uwezo wa kinga ya mwili
- Caffeine -caffeine kutoka kwenye vyanzo kama kahawa hupunguza maji mwilini
- Vinywaji vilivyosindikwa mfano soda- huongeza tindikali kwenye mwili
- Vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta
Tahadhari za kuchukua ili kuepuka madhara ya mkanda wa jeshi.
Pale juu tumeona kwamba mkanda wa jeshi hauambukizwi. Lakini virusi vyake vinaweza kusababisha tetekuwanga kwa mtu mwingine ambaye atagusa majimaji ya mgonjwa wa mkanda wa jeshi. Hivo kama wewe ni mgonjwa hakikisha unajifunika malengelenge yasionekane, na kuosha mikono kwa maji safi.
Unaweza kujaribu immune care package yetu kwa kubonyeza hapa ambayo itakusaidia
- Kuimarisha kinga ya mwili na kukusaidia kupona haraka ugonjwa wa Mkanda wa jeshi
- Kujenga na kuimarisha neva zilizoathiriwa na virusi wanaosababisha mkanda wa jeshi
- Kukuongezea Vitamin B na C na madini ya Zinc+Calcium ambazo zinaimarisha kinga ya mwili.
Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba :0678626254 kupata Huduma ya dawa kwa Tsh 165,000/= tu