Sickle cell anemia au Seli mundu ni aina ugonjwa wa kurithi ambao huathiri seli nyekundu za damu na vibeba oxygen kwenye damu vinavoitwa haemoglobin. Kutokana na kwamba ugonjwa huu ni wa kurithi hivo unaweza kuambukizwa kupitia kizazi kimoja hadi kingine.
Ifahamike kwamba sickel cell anemia ni aina mojawapo kati ya magonjwa ya siko seli. Lakini wenyewe huletekeza dalili mbaya zaidi na kuzorotesha afya ya mgonwa kama kuongezeka kwa maambukizi mbalimbali, homa kali na figo kushindwa kufanya kazi na matatizo mengine mengi kuliko aina zingine za siko seli.
Watu wengi wenye ugonjwa huu wa seli mundu/siko seli hupata upungufu mkubwa wa virutubisho katika mwili kutokana na uwezo mdogo wa kufyonza viini lishe kutoka kwenye chakula anachokula.
Siko seli anemia (seli mundu) ni ugonjwa gani?
Siko seli anemia ni aina ya ugonjwa wa kurithi ambapo hutokea pale mtu anaporithi gene beta-globin zilizoathirika kutoka kwa mzazi wake. Gene hizi zinaathiri moja kwa moja ufanyaji kazi wa seli nyekundu za damu.
Hameoglobin ni kitu gani
Kwanza ni muhimu kufahamu haemoglobini ni nini. Haemoglobin ni kiambata cha protein kilichopo kwenye seli nyekundu za damu. Kazi yake ni kubeba hewa safi ya oxygen kuisafirisha sehemu mbalimbali za mwili kupitia kwenye damu.
Kwa mgonjwa wa siko seli, seli zake nyekundu zinakuwa na umbo la mundu ama mwezi nusu. Kitu ambacho siyo cha kawaida kwani seli nzima huwa na umbo la mduara. Seli hizi za damu zenye umbo la mundu zinapata ugumu kusafiri kwenye mishipa ya damu kutokana na umbo lake.
Na ndipo hupelekea seli hizi kuvunjika na kukwama njiani kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kusafiri na hivo hewa safi ya oxygeni haifiki sehemu mbalimbali za mwili.
Aina za sickle cell
Kuna aina karibu tatu za siko seli, ikiwemo hii ya siko seli anemia. Watafiti wanasema siyo kwamba uwepo wa seli mundu baadhi zilizoathirka kwenye damu basi siyo kigezo kwamba seli zote nyekundu za damu zitakuwa na umbo la selimundu. Lakini kadiri muda unavosogea ndivo seli mundu nyingi zaidi zitakavoongezeka.
Seli nzima za damu huchukua siku 120 kufa lakini seli mundu hufa baada ya siku 20 tu. Jambo hili husababisha upungufu mkubwa wa damu kwa mgonjwa na pia kukosa hewa safi kwenye mwili.
Dalili na viashiria kwamba tayari una siko seli anemia.
Kama tulivosoma hapo juu, ugonjwa huu wa siko seli anemia unasababisha kukwama kwa damu kwenye mishipa ya damu. Hali hii husababisha maumivu na dalili zingine mbaya ambazo zinaathiri shuguli na viungo mbalimbali vya mwili kama figo, ubongo, mifupa, bandama na vingine.
Kila mgonjwa mwenye sikoseli anemia basi hupata upungufu wa damu mara kwa mara. Wagonjwa wengi wa siko seli hupata dalili zingine kama
- Uchovu mkali na mwili kuchoka sana
- Kupata homa kali mara kwa mara
- Kuvimba mwili na kujaa maji
- Kupata shida ya kupumua na maumivu ya kifua na hivo mgonjwa kushindwa kuwa mchangamfu
- Maumivu ya mifupa na joints,kupungukiwa kwa uroto (bone marrow) kwenye mikono na miguu na hivo kuleta maumivu makali
- Maumivu ya tumbo
- Matatizo katika kuona
- Kupata kizunguzungu, kutapika, na shida kwenye usagaji wa chakula
- Kuathirika kwa usafirishaji wa virutubisho na hewa kwenye damu husababisha Ngozi kupata malengelenge
- Ngozi kuwa ya njano kutokana na kuongezeka kwa nyongo kupita kiasi kwenye bandama.
- Wagonjwa wa siko seli wapo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi kama nimonia(pneumonia) kutokana na bandama kutofanya kazi vizuri
- Kushindwa kushiriki ngono ipasavyo, mfano wanaume hupata maumivu uume unaposimama.
- Pia wagonjwa wa siko seli wana hatari zaidi ya moyo kupanuka kutokana na kuongezeka kwa presha kusukuma seli za damu zilizokwama kwenye mishipa ya damu.
Kwanini watu huugua sickle cell anemia
Nini husababisha ikiwemo makundi ya watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata siko seli.
Kama tulivosoma hapo juu ugonjwa wa siko seli ni wa kurithi. Hivo hausababishwi na maingira au mtindo wa maisha. Kwa mtoto kupata siko seli lazima arithi baadhi ya gene zilizoathirika.
Kwahiyo kama mzazi mmoja ameaththirika, basi mtoto atarithi gene hizi lakini ugonjwa na dalili hazitajionesha mpaka pale huyu mtoto akipata mzazi mwenzake ambaye naye alibeba gene zilizoathirika basi mtoto atakayezaliwa atakuwa na siko seli anemia na dalili zake zitakuwa zinajionesha. Kwa hiyo kabla wazazi hawajapata mtoto wanaweza kufanya vipimo ili kujua kama wamebeba gene za siko seli.
Aina 5 za tiba asili kwa dalili za siko seli anemia.
Lishe na virutubisho vitakavyokusaidia kutibu dalili za siko seli
Tumeshaona pale juu kwamba ni vigumu kuzuia kupata sickle seli au kutibu siko seli lakini tunaweza kutibu dalili zinazotokea kwa mgonjwa husika. Watu wenye siko seli hupata taabu katika kumeng’enya chakula aina ya protini (amino acids) na hivo kupelekea utapiamlo, kupungua uzito kwa kasi na madhara mengine mengi. Hapa chini ni dondoo muhimu za kukusaidia ili kufikia lengo lako katika kuimarisha uwepo wa virutubisho vyote mwilini.
- Kula chakula mara kwa mara, hii itasaidia kufidia viini lishe ambavyo havijaweza kufyonza na mwili.
- Kula kwa wingi mlo kamili ambao una matunda na mboga mboga. Ongeza matunda yenye rangi na mbogamboga kwenye kila mlo ili upate vitamins, madini na viondoa sumu vya kutosha. Machaguo yako yawe, mboga zote za kijani, karoti, asparagus, nyanya, na uyoga.
- Kula protini za kutosha, madini ya chuma, na vyakula vya mafuta. Vyanzo vizuri vya protini na madini ya chuma ni nyama, mayai ya kienyeji, samaki na maini, uwepo wa madini chuma husaidia kupunguza athari za upungufu wa damu mara kwa mara. Vyanzo bora kwa vyakula vya mafuta ni kama nazi, mafuta ya nazi na mziwa ya nazi, mafuta ya mizeituni, karanga, mbegu, na parachichi
- Kula kwa wingi vyakula vyenye vitamin B complex (folate), ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Vyakula hivi ni pamoja na spinach, maini, viungo vya Wanyama kama moyo na figo, beets, maharage, lentils, parachichi, broccoli na asparagus, kutokana na ushauri wa dactari unaweza pia kupata vidonge vyenye virutubisho/supliments za folate, unaweza kujipatia kutoka kwenye stoo zetu japo lishe bora ndio silaha yako nzuri zaidi.
- hakikisha mlo wako 100% uwe wa asili yaani haujasindikwa, ikiwemo vinywaji vyote vya viwandani na vyenye sukari, (angalizo kama mwili wako unakataa ulaji wa wanga na nafaka basi unafaa kusitisha mara moja.
BAADHI YA VIRUTUBISHI VILIVYOPO KWENYE MFUMO WA VIDONGE AMBAVYO UNAWEZA KUNUNUA NA KUTUMIA NI PAMOJA NA
- Vitamin D: hakikisha pia unapata mwanga wa kutosha wa jua kila siku
- virutubishi vya Calcium
- Folic acid/folate
- Omega 3 fatty acids
- Vitamin B6 na B12 na
- Multivitamins zenye madini ya copper, zinc na magnesium.
- Punguza msongo wa mawazo na hakikisha unapata mda mwingi wa kupumzika: kama ni kufanya mazoezi basi ni yale mepesi ambayo hayatakuhitaji utumie hewa nyingi ya oxygen. Pata usingizi wa kutosha walau masaa 7 mpaka 8 kwa siku ili kusaidia mwili kurecover kutokanna na mazoezi na shuguli za siku nzima.
- Mwili wako uwe na oxygen ya kutosha na maji ya kutosha, epuka shuguli ngumu ambazo zinatumia oxygen nyingi kama kukimbia riadha na mazoezi makali ya jeshini.
- Tumia mafuta ya lazima i(essential oil) li kupunguza maumivu ya joints, tumbo, misuli, kifua na mifupa, mafuta haya ni kam Pepermint abayo unaweza kununua phamarcy. Usitumie vidonge vya kuungua maumivu kwani huleta madhara na kuzorotesha ufanyaji kazi wa figo na ini. Mgonjwa wa siko seli apewe huduma ya kwanza kwa kuwekewa kitu cha moto mahali panapopata maumivu makali mfano chupa ya plastic yenye maji ya moto.
- Mwisho jaribu kutumia virutubisho vinavyopatikana kwenye stoo yetu: virutubisho hivi ni kama.
Multivitamins kwa mgonjwa wa siko seli
kirutubisho hiki kilichojaa vitamin zote muhimu kama Vitmin A, B1, B2, B6, B12, C, D, Vitamin e na Folate, vitamsaidia mgonjwa wa sickle cell kuongeza vitamin ambazo zinapota kutokana na mwili kushindwa kufyonza vitamn hizi kama tulivoeleza athari za sickle sell pale juu.
Spirulina
Gramu 1 ya mimea ya spirulina ina lishe sawa na kilo 1 ya mboga na matunda. Ina kiasi kikubwa cha ferrous (mara 20 zaidi ya chakula cha kawaida chenye ferrous kwa wingi kama spinach).
Spirulina ina kiwango cha B12 mara 3.5 ya kile kilichomo ndani ya maini ya wanyama. Ina carotinoids mara 1.5 ya ile iliyomo ndani ya karoti. Kuna mlolongo wa vitamini B zikiwemo B12, vitamini K, na madini kama calcium, magnesium, selenium, manganese, potassium, na zinc.
Spirulina pia ni chanzo kikubwa cha selenium asilia, ambayo ni anti-oxidant yenye nguvu. Selenium hufanya kazi ikisaidiana na vitamini E kuhakikisha upatikanaji wa oksijeni ya kutosha kwenye misuli na haswa kwenye myocardium.
Kinga za mwili pia husaidiwa na selenium. Selenium pamoja na Vitamini E hulinda chembechembe nyekundu za damu, ngozi nyembamba inayozunguka seli na viungo vya seli kutokana na radikali huru. Na hivo kuwafaa zaidi wenye siko seli anemia. Kwa mgonjwa wa siko seli hutakiwi kukosa kirutubisho hiki, tembelea stoo yetu sasa.
Pine Pollen Tea
Pine Pollen ni namna ya chakula cha ziada cha kutunza afya chenye ufanisi wa hali ya juu. Inaweza kukuondolea uchovu haraka, kukuongezea nguvu, kupunguza tatizo la kukosa choo, kuboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, kutunza uimara wa ngozi na kuifanya ivutie, kukufanya uwe na furaha na mwenye nguvu na kuboresha kumbukumbu.
Mpaka sasa pine pollen imeshajizolea umaarufu katika nchi nyingi kama bidhaa muhimu ya afya kama Marekani, China na Canada. Sababu kubwa ni kuwa pine pollen inahuishwa na kuishi maisha marefu. Hukupa mtumiaji chakula kilichojitosheleza.
Madini adimu katika pine pollen, flavonoid, arginine , VC, VE, B-carotene na selenium vinaweza kuondoa radikali huru(free radicals) na hivo kuzuia uharibifu wa seli za damu. Kirutubisho hiki kinawafaa zaidi wenye matatizo ya kinga, siko seli na wanawake wenye matatizo ya homoni. Unaweza kupata kirutubisho hiki pia kupitia kwenye stoo zetu.
Soma makala inayofuata: