Kutoka Damu Puani
Tatizo la kutokwa damu puani linawapata watu wengi sana japo katika hao ni mara chache linaweza kuashiria kuna shida kubwa ya kiafya. Kwenye pua kuna mishipa midogomidogo mingi ya damu ambayo ipo mbele na nyuma ya pua. Mishipa hii ni laini sana na yaweza kupasuka na kuvuja damu kiurahisi.
Kuna aina mbili za utokaji wa damu. Aina ya kwanza damu inatoka kupitia matundu mawili ya pua(anterior nosebleed) na aina ya pili damu inavuja kwa ndani kuelekea kwenye koo(posterior nosebleed). Aina hii ya pili ni hatari zaidi, na yatakiwa kumwona daktari haraka
Nini Kinachosababisha Kuvuja damu puani?
Kuna vihatarishi vingi sana vinavyopelekea kutokwa na damu puani. Hata hivo unatakiwa kufahamu kwamba kuvuja damu puani kwa mara moja na kwa muda mfupi inaweza isiwe tatizo. Lakini kama unavuja damu puani mara kwa mara basi tambua kuna shida kubwa ya kiafya inayotakiwa kufuatiliwa kwa umakini.
Hewa Kavu
Hewa kavu isiyo na unyevunyevu ni chanzo kikubwa cha damu kuvuja puani. Watu wanaoishi kwenye mazingira ya joto kali wapo kwenye hatari zaidi kwani mishipa ya damu ya puani hupasuka na kuvuja damu puani kiurahisi.
Matumizi ya dawa zilizopo kwenye kundi la antihistamines na decongestants kwa aili ya aleji, sinus na mafua huweza kukausha kuta za ndani za pua na kusababisha mishipa kupasuka kiurahisi.
Sababu zingine za kuvuja damu puani ni kama
- Kukwama kwa kitu kwenye pua
- Alegi kutokana na kitu kigeni
- Kupata jeraha kwenye pua
- Kupiga chafya mara kwa mara
- Mazingira ya baridi sana
- Shinikizo kubwa la damu
- Tatizo la damu kutoganda haraka
- Saratani
- Maambukizi kwenye njia ya hewa na
- Matumizi makubwa ya dawa za asprin
Kwa kiasi kikubwa kuvuja damu puani inaweza isiwe tatizo linalohitaji tiba. Lakini unatakiwa kupata usaidizi wa daktari kama tatizo litaendelea kwa zaidi ya dakika 20. Dalili hii inaweza kuashiria pia damu inavujia kwa ndani kitu ambacho ni hatari zaidi.
Hatua gani za Kuchukua ikiwa Unavuja damu puani?
Tiba inatofautiana kwa kutegemea na aina ya utokaji wa damu kama tulivoelezea pale awali. Endelea kusoma kujua zaidi
Damu kuvuja kwa mbele kupitia matundu ya pua
Kama damu zinavuja kwa mebel kupitia matundu, jaribu njia hii ukiwa nyumbani. Wakati umekaa ziba mashimo ya pua kwa kubinya eneo laini la pua. Kisha shikilia wa dakika 10 wakati huo unavuta hewa kupitia mdomo.
Usilale kwa mgongo maana unaweza kumeza damu ikaleta shida tumboni.
Baada ya dakika 20 achia pua zako na jiangalie kama damu haitoki tena, kisha rudia zoezi kama bado damu zinatoka puani.
Unaweza pia kutumia kitu cha baridi mfano barafu ikiwa imewekwa kwenye mfuko kwa kuweka eneo la puani kwa dakika kadhaa. Muone daktari haraka kama uishindwa kuzuia kutoka kwa damu.
Kuvuja damu kwa ndani
Kwa kesi hii damu huvuja kushuka kwenye koo, na hutokea mara chache zaidi ulinganisha na aina ya kwanza. Aina hii ya kuvuja damu ni hatari na haitakiwi kutibia ukiwa nyumbani. Muone daktari haraka kama unahisi damu inavuja kwa ndani.
Kuvuja damu puani kutokana na kuingiliwa au kuchomwa ana kitu:
Kwa kesi hii daktari atasaidia kutoa kitu au kifaa kilichoingia puani na kusababisha kutokwa damu.
Namna ya Kujikinga Usivuje Damu puani
Njia zifuatazo zitakusaidia usipatwe na tatizo hili
- Acha kuvuta sigara. Kama wewe umekuwa mlevi wa sigara, kuacha matumizi ni jambo la muhimu ili kupunguza hatari ya kuvuja damu puani, sigara hukausha pua zako na pia kufanya tishu laini za ndnai ya pua zitutumke.
- Penga kamasi kwa taratibu: Usitumie nguvu kubw apake unapopenga makamasi, inaweza kusababisha kutokwa na damu puani
- Usiingize vidole puani kila mara: Vidole vinashika vitu vingi kwahivo kuviweka puani kila mara inaweza kuletekeza tishu laini za pua kututumka na hivo kutokwa na damu
- Piga chafya mdomo ukiwa wazi: inatokea mara nyingi ukiwa kwenye kundi la watu unapiga chafya kwa kuziba mdomo, ni hatari inaweza kusababisha presha kubwa kwenye mishipa ya damu ya kwenye pua, kupasuka na hivo kutokwa na damu.
- Tumia vyakula vyenye vitamin K kwa wingi: Vyakula hivi ni kama mboga za kijani kama spinach, vitunguu maji, matango, maziwa mtindi, kabeji na broccoli.
- Tumia kwa wingi vyakula vyenye vitamin C: kama Mapera, papai, machungwa, broccoli, Maembe,cauliflower, malimau na hoho nyekundu