Afya ya Mwanamke na Uzazi Salama
Kwanini hushiki ujauzito? Hizi ndizo sababu pamoja na hatua 3 za kusafisha kizazi chako na kurekebisha mpangilio wa hedhi.
Je unafahamu kwamba kusafisha kizazi ni hatua muhimu katika kuuandaa mwili kushika ujauzito?. Mfuko wa mimba ni kiungo kimoja cha ajabu chenye urefu wa sm 7 na upana wa sm 5. Kiungo hiki kimetengenezwa kwa muunganiko wa kuta tatu ambazo ni perimetrium(ukuta wa nje),myometrium (ukuta wa kati). Ndani ya myometrium kuna kuta zingine laini zilizotengenezwa kwa misuli.
Ukuta wa tatu ni endometrium(ukuta wa ndani).Ndani ya endometrium kuna tezi ambazo ndizo zinaratibu mpangilio wa hedhi. ukuta huu ndio humeguka na kutolewa nje kama hedhi pale mwanamke anapokuwa kwenye siku zake.
Sababu zinazopelekea Kizazi chako Kutofanya Kazi vizuri.
Kizazi chako kinafanya kazi muda wote ili kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kiumbe kitakachotungwa. Kazi hizi zinaratibiwa na mpangilio mrefu wa vichocheo ambavyo vinafanya kazi kwa kutegemeana. Kwa hivo kihatarishi chochote ambacho kinavuruga mpangilio huu kinafanya hata uwezo wa kushika mimba kupugua.
Zifuatazo ni sababu zinapekelea kuharibu afya ya kizazi chako na kuletekeza ugumba
Mtindo wa maisha
Wanawake wanaoishi pasipo kufanya mazoezi na kutumia mda mwingi wakiwa wamekaa, ama shughuli zisizoshugulisha mwili wanakuwa kwenye hatari zaidi ya kupungua uwezo wa kushika mimba. Maisha haya ya kizembe hupelekea kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye via vya uzazi. Kutoshughulisha mwili pia kunapunguza uwezo wa misuli ya kizazi na hivo kupunguza uwezo wa kuhifadhi ujauzito.
Uvimbe wa fibroid kwenye kizazi
Uvimbe huu hufanyika mara nyingi kwenye kuta za kizazi na kusababisha maumivu makali wakati wa hedhi. Dalili zingine ni kupata hedhi nzito na inayochukua mmda mrefu na maumivu ya nyonga. Unaweza kusoma zaidi kuhusu uvimbe wa namna hii na namna ya kurekebisha lishe ili kupona. Bofya hapa kusoma zaidi makala ya fibroids.
Makovu kwenye kizazi
Makovu haya kwenye kizazi yanaweza kufanyika kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizi kama zilivoelezewa kwa msaada wa Chuo kikuu cha California, shule ya udaktari ni pamoja na
- mimba kuharibika
- utoaji wa mimba
- upasuaji wakati wa kujifungua
- matumizi ya kitanzi ili kuzuia mimba
- kuugua magonjwa ya zinaa na PID
- uvimbe kwenye ukuta wa ndani wa kizazi (endometriosis)
Wanawake waliowahi kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi wapo kwenye hatari zaidi.
Kuvurugika kwa homoni
Homoni zinafanya kazi kubwa katika kuratibu utendaji wa shughuli za mwili kwenye kizazi. Homoni zinapovurugika hupelekea matatizo kama uvimbe kwenye kizazi (endometriosis na fibroids ) na uvimbe kwenye mayai (Polycyst ovarian syndrome)
Utagunduaje kama vichocheo vyako vimevurugika. Angalia uwepo wa dalili hizi
- hedhi kuvurugika
- kupata hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku 5
- uzito mkubwa na kitambi
- kuota ndevu
- maumivu makali ya tumbo kipindi cha hedhi
- kukosa hamu ya tendo la ndoa na
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
Kizazi kuinama
Kikawaida kizazi kinatakiwa kuwa kimenyooka upande wa juu na chini pale mtu akiwa wima. Kutokana na sababu mbalimbali inaweza kupelekea kizazi kuinama kuelekea nyuma au mbele. Tazama picha hapa chini
Kizazi kinaweza kuinama kutokana na kutanuka kwa kwa misuli baada ya kujifungua, makovu na uvimbe kama fibroids na endometriosis. Kizazi kilichoinama kinaweza kuleta dalili kama maumivu makali, kuvurugika kwa hedhi, kuugua UTI mara kwa mara, ugumu kwenye kuvaa pedi na pia maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Jinsi gani uimarishe afya ya kizazi?
Hapa chini ni maelezo ya jumla namna ya kurekebisha mtindo wako wa maisha ili kuimarisha afya ya kizazi. Kama una magonjwa kama fibroids, ovarian cysts na kuziba kwa mirija hakikisha unapitia makala zake ambazo tayari tumeshaziandaa hapa kwenye website yetu.
- Mazoezi: Hii ni hatua ya kwanza kabisa kuelekea kwenye kusafisha kizazi chako. Mazoezi ya kutembea na Yoga ni mazuri zaidi hata kama wewe ni mvivu wa kwenda gym au uwanjani, yanasaidia kuimarisha mzunguko wa damu na unyumbulikaji wa misuli kwenye kizazi.
- Self Fertility Massage: Kufanya msaji eneo ya tumbo chini ya kitovu pande zote kulia na kushoto ni njia moja rahisi ambayo unaweza kuifanya ukiwa nyumbani pasipo gharama. Masaji ya tumbo inasaidia
- Kuimarisha mzunguko wa damu kwenye kizazi,ovari na mirija ya uzazi
- Kusaidia uwiano wa vichocheo
- Kuongeza uwezo wa kizazi kujisafisha kwa kutoa tishu zilizokufa na damu ya hedhi
- Kuimarisha usambazaji wa hewa safi ya oksijeni kwenye kizazi na Kuimarisha misuli ya kizazi.
- Fertility cleanse
Fertility cleanse ni moja ya njia nzuri ya kusafisha kizazi na kurekebisha homoni zako kwa kuimarisha uwezo wa ini.Ini ni kiungo kinachochuja sumu kwenye mwili, sumu hizi hujumuisha homoni zilizozidi ambazo zinaweza kupelekea kuvuruga mpangilio wa homoni.
Fertility cleansing pack pia inajumuisha kusafisha mfuko wa mimba kwa kutoa mabaki ya tishu na damu illiyoganda ambazo hazikutolewa kipindi cha hedhi. Hatua hii inatumia Dawa asili (herbs) na virutubisho ili kusapoti afya ya kizazi na kuimarisha mzunguko wa damu.
Green Health Fertility Cleansing Pack.
Package yetu ya Green Health Fertility cleansing inajumuisha
Uterine cleanse phase; ambapo utapata vidonge kwa ajili ya kusafisha kizazi na kuimarisha uzuri wa uke. Vidonge hivi ni vya kuweka ukeni kila baada ya siku tatu. Hatua hii inachukua jumla ya siku . Dozi hii hurudiwa mara mbili yaani jumla wiki mbili ili kuhakikisha unapona kabisa.
Green health fertility cleansing pack inawafaa wanawake wote wenye matatizo ya
- uvimbe kwenye kizazi
- uvimbe kwenye mifuko ya mayai (ovarian cysts)
- maambukizi sugu na PID
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
- kuziba kwa mirija ya uzazi na
- kutokwa na uchafu wenye harufu ukeni
Gharama ya Uterus cleansing pills Ni sh 50,000/= kwa dozi moja. Mgonjwa atashauriwa kutumia dozi mbili.
Angalizo pale unapotumia Uterus cleansing Pack; Makundi haya hawaruhusiwi kutumia
- wanawake wenye ujauzito
- wanawake waliopo kwenye hedhi
- wawake bikira
Kulingana na ukubwa na aina ya changamoto ya mgonjwa, tunaweza kupendekeza utumie zaidi ya dozi moja ili kupona.
angalizo
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.