Categories
Dondoo za afya

Kutokwa Jasho Jingi lenye Harufu

kutokwa jasho jingi

Maelezo ya utangulizi

Ni kawaida kila mtu anatokwa na jasho kweye mwili. Kutokwa jasho ni hali ya mwili kujipooza na kuzuia kupanda kwa joto la mwili kupita kiasi. Kwahivo mwili unapopambana kubalansi joto lako la mwili ndipo hapo utaanza kutokwa na majasho. Inapotokea unapata jasho jingi na linatoka pasipo joto la ndani ya mwili kuongezeka hapo ndipo tunasema una tatizo, ambalo kitaalamu linaitwa hyperrhidrosis.

Watu wenye tatizo hili hutokwa na jasho jingi kipindi ambacho mwili hauhitaji kupoozwa.
Tatizo hupunguza sana hali ya mtu kujithamini kwasababu linakera na kusumbua. Dalili za jasho jingi zinatofautiana kwa watu na ni tatizo
la kurithiwa kwa vinasaba kutoka kizazi kimoja hata kingine. Tatizo hili tunaweza kuligawanya katika makundi mawili

Primary Hyperhidrosis

Aina hii ya kutokwa jasho jingi huanzia utotoni au kipindi cha balehe na hutokea kwenye maeneo kadhaa ya mwili hasa kwenye miguu, paji la uso na kwenye kwapa. Mara nyingi kwa kesi hii mtu huaanza kutokwa jasho jingi baada tu ya kuamka kitandani.

Secondary Hyperhidrosis

Aina hii ni pale mtu anapotokwa na jasho jingi mwili mzima na unaweza kupata dalili hizi hata kama umelala. Chanzo chake yaweza kuwa tatizo flani la kiafya linalokusumbua au matumizi ya dawa.
Hali ya jasho jingi inakera na yaweza kukukwamisha kufanya shughuli zako za msingi mfano kufungua kurasa za kitambu, kufungua mlango au kushukilia kitu.

Sababu na vihatarishi vinavyopelekea mtu kutokwa jasho jingi ni pamoja na

  • Kuugua kisukari
  • Kukoma hedhi
  • Maambukizi
  • Msongo wa mawazo
  • Ugojwa wa gauti
  • Tezi ya pituitari kufanya kazi zaidi (hyperpituitarism)
  • Ujauzito
  • Athari ya sumu kama metali nzito mfano mercury
  • Uzito mkubwa na kitambi
  • Uvimbe
  • Kushuka kwa kiwango cha sukari kuliko kawaida kwenye damu (hypoglycemia)
  • Matumizi vyakula na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa
  • Matumizi ya aina fulani za vidonge
  • Kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya kuugua tatizo hili na
  • Pombe

Hatua 3 za Kutibu na Kupunguza kutokwa jasho jingi.

  1. Weka mwili katika hali ya usafi muda wote
    Hakikisha unaosha vizuri na kukausha miguu inayonuka,kwapa zenye jasho na maeneo mengine ya mwili zenye athari. Ili kuzia maambukizi kwenye ngozi yenye unyevunyevu hakikisha unatumia sabuni zilizotengenezwa kwa siki au vinegar ya apple au mafuta ya tea tree, na witch hazel, yatasaidia kuzuia maambukizi ya fangasi na bacteria kwenye ngozi.
  2. Vidonge vya Soy power na Zinc kwa wanawake
    Kama chanzo cha tatizo lako ni kukoma hedhi, basi hakikisha unatumia vidonge vya Soy power na zinc viakusaidia kupunguza dalili za kukoma hedhi kama kutokwa ana jasho usiku na mwili kuchoka sana unaweza kuagiza hapa.
  3. Jaribu njia mbalimbali za kupunguza msongo wa mwanzo, kwa kufanya mazoezi kama yoga, tahajudi (meditiation)

ANGALIZO

Kutokwa jasho jingi yaweza kuwa siyo tatizo kubwa lakini linaweza kuathiri uwezo wako wa kufanya shughuli za kimaisha.Kwa nyongeza kama tulivoona pale awali kupata jasho jingi inaweza kusababishwa na tatizo kubwa la kiafya ambalo unatakiwa kushughulika nalo, kama kisukari, uvimbe na athari ya sumu kama metali nzito.
Unapotumia njia kama marashi, au pafyumu ili kupunguza harufu na wingi wa jasho basi hakikisha unasoma kwanza kuhusu athari zake.a

Share and Enjoy !

Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shares