Tiba ya Kukosa choo Pamoja Na Lishe Yake.
Unapata shida ya choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu? Basi fahamu kwamba haupo peke ako maana kuna kundi kubwa la watu wanapata shida hiyo kila siku. Constipation ni tatizo linalokosesha wengi raha na linaathiri mamilioni ya watu duniani kote. Tatizo likiwaathiri zaidi wanawake kuliko kundi lingine lolote.
Licha ya kuleta usumbufu ukiwa chooni, constipation huleta shida zingine kama tumbo kujaa gesi, kuhisi umeshiba mda mwingi, na pia uchovu na msongo wa mawazo. Kila siku mamilioni ya watu wanatumia pesa nyingi katika kununua dawa kwa tatizo hili.
Habari njema ni kwamba tatizo hili unaweza kuliepuka na kuna tiba asili nyingi sana kwa tatizo hili ili kusafisha tumbo lako na kupunguza athari unazopata. Kwnye makala hiiutajifunza namna ya kuepuka tatizo hili ili uepuke kupoteza pesa zako na kuitibu ukiwa nyumbani.
Constipation Ni Nini?
Constipation inalezwa kwamba ni ugumu wa kutoa uchafu wote kwenye tumbo, hii ni kutokana na choo kuwa kigumu. Kwa maaana nyingine ni kwamba ni hali ya kupungua kwa kasi ya utoaji kwa uchafu/kinyesi tumboni ama kupata choo kigumu na kukosa choo kwa muda mrefu.
Nini Husababisha Constipation/ Kukosa Choo Au Kupata Choo Kigumu?
Umewahi kujiuliza kwanini unakosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu na kwa shida, huku ukipata maumivu makali wakati wa kujisaidia? Kwa kiasi kikubwa kukosa choo na choo kigumu husababishwa na mkusanyiko wa sababu.
Sababu hizi ni pamoja na lishe yako, kiasi gani mwili wako unaushugulisha, na na jinsi unavocontrol stress/msongo wa mawazo. Sababu kubwa kabisa ikiwa ni ulaji wa vyakula vyenye kiwango kidogo sana cha kambakamba/fibers na matumizi kidogo ya maji .
Unapopata constipation baadhi ya dalili huanza kujitokeza kwenye mfumo wa chakula kama; kupungua wa kasi ya utoaji wa kinyesi au uwepo wa kiasi kidogo cha kinyesi, kuchelewa kwa utolewaji wa kinyesi kuliko kawaida. Kama unaumwa magonjwa kama Irritable bowel syndrome (IBS) au ugonjwa mwingine kwenye mfumo wa chakula basi yaweza kuwa ndio chanzo cha constipation.
Sababu za kukosa choo na choo kigumu
Hapa chini ni sababu zinopelekea upate constipation
- Lishe mbovu: Vyakula vilivyosindikwa sana, sukari, nafaka iliyokobolewa, pombe. Vyakula vilivyoongezwa sukari na kemikali za kutunza chakula kisiharibike na mafuta mabaya huleta ugumu kwenye utengenezaji na utolewaji wa kinyesi na hivo kukupelekea kukosa choo kwa muda mrefu.
- Msongo wa mawazo: Watu wanaopata msongo mkubwa wa mawazo huharibu mpangilio wa homone zao pamoja na kuathiri uzalishaji wa visambaza taarifa kwenye mwili na hivo kusababisha shida kwenye misuli, kupata mcharuko/mpambano ndani ya mwili (inflammation) na kuathiri ufanyaji kazi wa enyzmes ambazo husaidia kumeng’enya chakula.
- Kutoshughulisha mwili: Mazoezi yanasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mfumo wa chakula na kuimarisha misuli na hivo kurahisisha utolewaji wa kinyesi. Utafiti unasema watu wanaotumia mda mwingi wakiwa wamekaa hasa maofsini wanaongoza kwa kuapata matatizo ya kukosa choo kwa mda mrefu.
- Matumizi ya baadhi ya vidonge: Baadhi ya vidonge husababisha kukosa choo kwa muda mrefu na kupata choo kigumu. Mfano dawa za kupunguza maumivu, dawa za kuconrtol stress, dawa za kulevya, virutubisho vya calcium na magnesium na antiacids.
- Ukuaji wa bacteria wabaya kwenye mfumo wa chakula: Bacteria wazuri/normal flora waliopo kwenye mfumo wa chakula tunawaita probiotics husaidia kwenye uchakataji wa chakula. Ndio maana kuna umuhimu wa kula vyakula vyenye kambakamba kwa sababu ni mbolea nzuri kwa bacteria wazuri kukua na kufanya kazi.
- Matatizo ya tezi ya thyroid na matatizo mengine ya homoni: Matatizo kama kisukari, kukoma hedhi, maumivu kabla ya hedhi na ufanyaji kazi hafifu wa tezi ya Thyroid huweza kusababisha kupata constipation. Magonjwa mengine ni kama Pakinson disease, ajali ya uti wa mgongo na matatizo mengine ya neva yanaweza kusababisha Constipation.
- Upungufu wa magnesium: magnesium husaidia ufanyaji kazi mzuri wa misuli na hivo kusaidia utolewahi mzuri wa kinyesi.
- Baadhi ya tabia hatarishi wakati umeenda chooni: tabia hizi ni kama kujisaidia kwa haraka na ukaaji mbaya unapokuwa chooni huchangia kuongeza ukubwa wa tatizo na kisha kupelekea kupata ugonjwa wa bawasili
- Umri mkubwa na kukosa usingizi huchangia pia kukosa choo kwa muda mrefu
Dalili za Constipation
- Kupata choo kidogo zaidi kuliko kawaida au kukosa choo kwa muda mrefu; kumbuka hakuna kipimo kimoja kwa wote, hii inatofautiana kwa kila mtu, kuna watu huenda zaidi ya mara moja chooni kwa siku, na wengine huenda chooni mara moja tu kwa siku. Cha kuzingatia ni kuangalia choo chako na kuchunguza kula unapojisaidia, kumbuka usiwahi kufalsh choo chako unapomaliza, chunguza fanya ulinganifu kama choo kinaashiria una afya nzuri ama umeanza kuumwa.
- Kupata choo kigumu na kuwa na maumivu wakati wa kujisaidia na wakati mwingine kukufanya utumie nguvu kubwa wakati wa kujisaidia.
- Tumbo kujaa gesi na kuhisi umeshiba mda mwingi wakati huajala na una njaa.
Tiba Ya Lishe Kwa Tatizo La kukosa choo na choo kigumu
Kwa mgonjwa unayekosa choo kwa muda mrefu unapoanza safari ya kutibu constipation kwa kutumia lishe basi kumbuka kufahamu vyakula gani ule kwa sana, vyakula gani usile, na virutubisho gani utumie na pia baadhi ya mtindo wa maisha kurekebisha ili ujizuie kupata constipation na utibu ukiwa nyumbani mwako.
Vyakula kwa ajili ya mgonjwa wa constipation ni
- Vyakula vyenye kambakamba/fibers kwa wingi: Kwenye mlo wako weka vyakula vingi vyenye kambakamba au nyuzinyuzi mfano karanga, nafaka isiyokobolewa, maharage, mboga za majani, na mbegu. Parachichi, broccoli, apple na viazi vitamu
- Mbogamboga za kijani: licha ya kuwa na kambakamba nyingi kwenye mboga za kijan, pia kunamdini mengi ya magnesium ambayo tumeona hapo juu husaidia katika ufanyaji kaz mzuri wa misuli na hivo kupunguza tatizo la constipation.
- Tumia kinywaji cha uvuguvugu: kama una tatizo la constipation jaribu kutumia chai ya moto asubuhi, au tumia maji yaliyochanganywa na limau, chai ya kuding kutoka china ni nzuri zaidi unaweza kuipata ofsini kwetu, inakusaidia kutibu tatizo hili haraka kwa sababu imeongezwa mimea tiba mingi.
Vyakula vya kuacha kabisa kutumia kwa mgonjwa ni pomoja na
- Vyakula vilivyokaushwa kwenye mafuta
- Pombe
- Vyakula na vinywaji vilivyopikwa kwenye joto kali sana mfano maziwa yaliyosindikwa
- Unga uliokobolewa na kusafishwa kupita kiasi
- Vinjwaji vyenya caffeine kwa wingi kama kahawa na baadhi ya chai.
Tiba Kupitia Dawa ya *CLEAR*
Clear ni dawa asili iliyo kwenye mfumo wa unga/powder, imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kutibu changamoto mbalimbali kama kukosa choo na kupata choo kigumu na gesi tumboni.
Namna ya Kutumia Clear.
Kutibu kukosa choo au choo kigumu, chemsha maji kidogo, kisha weka kwenye kikombe cha chai. Mimina unga wa clkear pakiti moja kwenye kikombe kimoja cha chai, koroga kwa dakika mbili kisha kunywa taratibu. Tumia hivo kwa siku sita. Kila siku tumia pakiti moja pekee na ukimaliza tumbo lako litakuwa safi, na choo utaanza kupata vizuri tangu siku ya kwanza ya dozi. Bei ya dozi moja ya clear kwa siku 6 ni Tsh 50,000/= unapona kabisa.