Majimaji Kwenye Matiti
Tatizo la kutokwa majimaji kwenye matiti huwapata zaidi wanawake walio na uwezo wa kushika mimba, kuanzia miaka 16 mpaka 40. Wanawake wanaweza kutokwa na majimaji kwenye matiti hata kama hawanyonyeshi na hawana mimba.
Dalili hii ya kutokwa majimaji inaweza kuwa sio ishu na hupotea kwa muda mfupi. Lakini kama ikiendelea basi yaweza kuwa ni dalili ya saratani ya matiti na unatakiwa kumwona daktari haraka.
Endelea kusoma zaidi kuhusu aina ya majimaji na ujue lini unatakiwa kumwona daktari.
Aina za Majimaji Yanayotoka kwenye matiti na chanzo cha tatizo
Majimaji kwenye matiti huja kwa aina tofauti za rangi, na hichi ndio kiashiria cha kukusaidia kujua chanzo cha tatizo lako. Jedwali hapa chini limeainisha rangi ya majimaji pamoja na chanzo chake.
Rangi | Kisababishi |
Nyeupe, mawingu, au njano | Maambukizi kwenye chuchu |
Kijani | Uvimbe (cyst) |
Majimaji Mn’gao | Saratani ya matiti na hasa kama majimaji haya yanatoka kwenye titi moja |
Damu | Saratani au maambukizi ya virusi wa papiploma |
Kumbuka pia majimaji haya yanaweza kuwa mazito na mepesi, au yanayonata. Na pia majimaji yanaweza kuwa yanatoka yenyewe au mbaka kupinya matiti. Na yanaweza kutoka kwenye titi moja au matiti yote mawili.
Dalili zingine Hatarishi
Dalili hizi zaweza kuambatana na kutokwa maji ni kama
- Maumivu kwenye matiti na matiti kuwa laini
- Uvimbe kwenye eneo la chuchu
- Chuchu kutengeneza mbonyeo (dimple), kubadilika rangi na kuwasha
- Titi kuwa na wekundu
- Mabadiliko ya umbile la titi mfano titi moja kuwa kubwa kuliko jingine
- Homa
- Kukosa hedhi
- Kizunguzungu na kutapika na
- Mwili kukosa nguvu
Nini hasa Sababu ya Kutokwa na Majimaji kwenye Matiti
Tunafahamu kwamba mwanamke akiwa mjamzito au ananyonyesha ni kawaida kutokwa maziwa kwenye matiti. Hali ya kutokwa na maziwa inaweza kuendelea kwa mwanamke kwa muda wa miaka mitatu baada ya kuacha kunyonyesha.
Kwa wanawake ambao hawanyonyeshi wala kuwa na mimba wanaweza kupata majimaji ambapo visabaishi vyake ni kama
- Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi
- Maambukizi kwenye tezi za matiti
- Mambukizi ya virusi wa papilloma
- Kutumia dawa za zinazoongeza uzalishaji ya homoni ya maziwa
- Msisimko mkubwa kwenye titi au chuchu
- Vimbe kwenye titi
- Mabadiliko ya homoni wakati wa hedhi au baada ya kukoma hedhi(menopause)
- Kuziba kwa mrija wa maziwa (mammary duct ectasia)
- Uvimbe usio saratani kwenye tezi ya pituitary(prolactoma) ambapo huchochea uzazlishaji kwa wingi wa homoni ya maziwa
- Kushuka kwa uwezo wa tezi ya thyroid na
- Saratani ya matiti
Uhusiano kati ya Kutokwa na Maji Kwenye Matiti na Saratani.
Moja ya dalili ya saratani ya matiti ni kutokwa na majimaji. Kama una saratani njia rahisi ya kugundua ni pale majimaji yanapotoka titi moja pekee. Pia saratani inaweza kuonekana kama kitu kigumu kilichojikusanya mahali pamoja.
Muda gani wa kumwona Daktari
Ni muhimu kumwona daktari endapo utapata dalili hizi ambazo ni kiashiria cha saratani
- Uvimbe kwenye titi
- Rangi ya chuchu kubadilika
- Kama majimaji yanakuwa na damu
- Endapo majimaji yanatoka kwenye titi moja pekee
- Kama majimaji yantoka bila kukoma
Tumia breast care tea kutibu changamoto za matiti yako
Kazi na faida za breast care tea
- Kutibu shida ya kutokwa na majimaji na maziwa kwenye matiti
- Kutibu chuchu na matiti yanayouma na kuvimba mara kwa mara
- Kuimarisha mzunguko wa damu kwenye matiti na kuondoa damu iliyoganda. Damu kuganda kwenye mishipa ndio chanzo kikubwa cha uvimbe kwenye matiti.
- Kukukinga dhidi ya changamoto za matiti kama saratani
- Kuzuia kujitokeza kwa saratani baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye matiti na
- Kuongeza kinga ya mwili