Jinsi ya kupata Mimba Mapacha

mimba mapacha
mapacha wanaofanana

Mimba ya Mapacha

Kwa miaka ya hivi karibuni wanawake wamekuwa wakichelewa sanaa kuanza familia ukilinganisha na miaka ya zamani,ambapo wanawake walikuwa wanaolewa wadogo mpaka miaka 15 wanaanza kujifungua.

Kutokana na hili wanawake kuzaa mapacha imekuwa zaidi kuliko zamani, kwasababu chansi ya kuzaa mapacha ni kubwa kwa wanawake wa umri zaidi ya miaka 35 na waliopata ujauzito kwa kutumia dawa zaidi(fertiliy treatment).
kama nawe unataka kuzaa mapacha fahamu kwamba hakuna formula moja kamili ya kufuata lakini kuna baadhi ya njia unaweza kurekebisha ili kuongeza chansi ya kushika mimba ya mapacha. Fuatana nami na mwisho wa makala utaweza kuamua kama ujaribu bahati yako au la…

Mimba ya Mapacha hupatikanaje?

Mimba hutungwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la mwanamke na kulirutubisha. Kama kwa kipndi ambacho mke na mume wamekutana kuna mayai mawili yametolewa au yai moja liliorutubishwa kugawanyika kuwa mawili basi mwanamke hupata mimba ya mapacha.

Ainza za Mapacha

Mapacha wanaofanana (identical twins): aina hii ya mapacha hufanyika endapo yai moja liliorutubishwa kugawanyika vipande viwili. Mapacha hawa hufanana vinasaba, sura na jinsia pia.

Mapacha wasiofanana(fratenal twins): Aina hii ya mapacha hutokea pakiwa na mayai mawili yaliyokomaa kwenye kizazi wakati wa urutubishaji, na mbegu za kiume kurutubisha mayai yote mawili. Mapacha hawa wanakuwa na jinsia na vinasaba tofauti.

Kwanini mwanamke anajifungua mapacha, nini hutokea?

Mpaka sasa hakuna sababu za moja kwa moja kuonesha ni jinsi gani mpaka mapacha wanafanyika. Japo baadhi ya sababu huweza kuongeza chansi ya kupata mapacha, sababu hizi ni kama

Umri wa Mwanamke

Tafiti zinasema kwamba wanawake wenye umri mkubwa hasa kuanzia miaka 35 wana chansi kubwa ya kupata mapacha wasiofanana. Hii ni kwa sababu ovari za mwanamke huanza kutoa yai zaidi ya moja kila mwezi katika umri huo. sababu ingine ni kwamba wanawake wa umri mkubwa hutoa kichocheo cha FSH(follicle stilumating hormone kwa wingi) ambacho kazi yake ni kuchochea upevushaji wa mayai.

Familia kuwa na Historia ya Kuzaa Mapacha

Kama kwenye familia yako kama mwanamke ama kwenye familia ya mwanaume kuna mapacha basi una uwezekano mkubwa wa kupata mimba ya mapacha pia.

Kuwa kwenye tiba za kuongeza upevushaji wa mayai

Tiba za changamoto za uzazi ni njia maarufu sana kwatika kushika mimba ya mapacha. Vidonge vya tiba hizi huchochea uzalishaji wa mbegu za kiume na mayai ya mwanamke. Kama mayai mengi yakizalishwa kuna uwezekano kwamba yai zaidi ya moja litakuwa tayari kwa urutubishaji kuongezeka na hivo mimba ya mapacha kupatikana.

IVF(invitro fertilization)

IVF ni njia ya maabara ambapo daktari anatoa yai kwenye kizazi na kisha kupandikiza mbegu ya kiume nje ya kizazi kisha kiumbe kupandikizwa kwenye kizazi tena ili kukua. Njia hii ni ghali na wachache huweza kumudu Gharama zake zaweza kufikia sh milioni 24 za kitanzania.

Muhimu pale unapojaribu bahati yako kupata mapacha kupitia huduma yetu.

  • Pumzika kwa muda mrefu kati ya mimba moja na nyingine. Hii itasaidia mayai kutengenezwa kwa wingi na hivo kuongeza uwezekano wa kupata mapacha.
  • Wenza wote mke na mume wanatakiwa kutumia virutibisho, hivyo ni vyema kushirikishana katika hili ili muweze kushirikiana kufanikisha zoezi.
  • Huduma hii siyo ya uhakika kwa 100% hapana, ni jambo la kuongeza uwezekano , kadiri unavozingatia maelekezo yetu na kutumia virutubisho ndivyo unaongeza uwezekeno wa kupata mapacha
  • Kama una changamoto za uzazi inabidi tukupatie tiba kwanza kabla hujaanza hili zoezi.
  • Zoezi hili litawafaa zaidi wanawake wa umri kuanzia miaka 35 na kuendelea

Bofya kusoma kuhusu: Vyakula na mazoezi ya Kuongeza makalio

Share and Enjoy !

Shares
Shares