Bawasiri yaweza kuwa moja ya topic ngumu sana kuzungumziwa kiuwazi na watu. Hii ni kutokana na wagonjwa wengi kuona aibu pengine ni kwasababu tatizo husika hutokea mahala pa haja kubwa.
Wengine huona aibu hata kueleza tatizo hili kwa daktari ama muhudumu wa afya. Bawasili ni tatizo kubwa linawatokea wanaume kwa wanawake. Naweza kusema uwepo wa tatizo hili si ajabu ukiangalia wengi wetu wanakula vyakula zaidi vilivyosindikwa, hawafanyi mazoezi na wana msongo wa mawazo uliokithiri.
Je, Unajua Bawasiri/Hemorrhoids Ni Nini?
Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.
Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita hemorrhoids na kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles.
Tatizo la bawasili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50.
Aina Za Bawasiri
Kuna Aina kuu mbili za bawasiri
(A) Bawasili ya ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili,.Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
(1)Daraja la kwanza -Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika
(2)Daraja la pili -hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.
(3)Daraja la tatu-hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.
(4)Daraja la nne-hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.
(B)Bawasili ya nje
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu. Pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha aina ya bawasiri iitwayo thrombosed hemorrhoids.
Nini Chanzo Cha Bawasiri?
Bawasili kwa kiasi kikubwa huletekezwa na kuongezeka kwa mganadamizo ama presha mara nyingi ni pale unapojikaza ili kutoa haja kubwa. Hivo bawasili huwatokea zaidi watu wenye matatizo ya mfumo wa umen’gemnyaji, mfano unapata choo kigumu, tumbo kujaa gesi, kukosa choo kwa siku kadhaa.
Wamama wenye ujauzito pia huwa kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mtoto aliye tumboni kugandamiza tumbo la chakula na hivo kuathiri utoaji wa haja kubwa. Kwa bahati nzuri bawasili inayosababishwa na ujauzito huanza kuisha pale tu mama anapojifungua.
Watu wenye kitambi na uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mwili kushindwa kutengeneza nishati ya kutosha kusukuma uchafu kwenye utumbo.
Unagunduaje Kama Tayari Una Bawasiri
Wakati mwingine inatokea unaweza kuwa na bawasili lakini usipate dalili na baada ya mfupi ugonjwa huweza kupotea wenyewe. Dalili moja kubwa ambayo wagonjwa wetu wengi huipata kwa wenye bawasili ya ndani ni kuvuja kwa damu inayoweza kuonekana kwenye toilet paper ama kinyesi.
Unapoona dalili kama hizi hakikisha unachukua hatua za haraka maana tayari umepata bawasiri. Kama una bawasiri ya nje basi unaweza kupata viashiria kama uwepo wa nundu nyekundu iliyojaa damu pembeni mwa mahala pa haja kubwa, kitaalamu huitwa thrombosed hemorrhids .
Huambatana na maumivu makali sana wakati wa kutoa haja. Kama utoaji wako wa haja ni wa kujikamua na kwenda haraka haraka, na kujisafisha kupita kiasi basi unaweza kuongeza tatizo, ianashauriwa kutotumia nguvu kubwa kujisaidia.
Angalizo (Siyo Kila Unapoona Kuna Damu Inavuja Ni Bawasili)
Unapoona kuna damu inavuja mahala pa haja kubwa ama unapotoa haja, nashauri nenda haraka hospital kuonana na Dactari na kufanya vipimo. Hasa kama tatizo ni limekutokea kwa mara ya kwanza. Kuvuja kwa damu kwenye sehemu ya haja kubwa inaweza kuwa ni dalili za Saratani ya utumbo mpana .
Kitu kimoja cha kuvutia sana ni kwamba uwepo wa Vitamn D ya kutosha mwili hupunguza hatari ya kupata bawasili kwa karibu 80%. Kwahiyo kama tatizo linajirudia mara kwa mara basi fanya checkup kujua kama una vitamn D ya kutosha. Pia unaweza kutembelea stoo yetu ya virutubisho kwa kubonyeza hapa kupata kirutubisho chenye vitamin zote.
Vihatarishi/ Visababishi Vingine Vya Tatizo La Bawasiri
- Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
- Kuharisha kwa muda mrefu
- Kukaa kitako kwa muda mrefu
- Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu
Dalili zingine za zitakazokusaidia kugundua kama una tatizo la bawasili ni;
- Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
- kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
- Kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
- Kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
- Kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
Hatua Nne Za Kuzuia Kutokea Kwa Bawasiri
Hapo juu tumeona kwamba chanzo kikubwa cha tatizo hili ni matatizo ya mfumo wa umen’genyaji kama kukosa choo kwa mda mrefu, kupata choo kigumu, kuharisha mara kwa mara na tumbo kujaa gesi, hivo kwa kuzuia matatizo haya basi utakuwa umejikinga na bawasili. Hivo hakikisha unafanya yafuatayo;
- Kula mbogamboga za majani, na nafaka zisizokobolewa, matumizi ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi husaidia kuongeza ukubwa wa kinyesi na hivo kurahisha utolewaji wake, kama mwanzo hukutumia vyakula vya nyuzinyuzi basi anza kuongeza taratibu kwenye mlo wako mpaka pale tumbo litakapozoea.
- Tumia machungwa kwa wingi, machungwa yana kiungo kinachoitwa flavonoids, kiungo hiki ni muhimu katika ustawi wa mishipa ya damu ya Veins, mishipa hii ndio huathirika na kuletekeza bawasiri.
- Kunywa maji ya kutosha kila siku, tumia kiu na rangi ya mkojo kama kiashiria cha kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa, kama mkojo ni wa rangi ya njano inayokolea basi ni kiashiria kwamba mwili hauna maji ya kutosha na unatakiwa kunywa. Nyuzinyuzi na maji ya kutosha husaidia kulainisha choo chako na hivo kurahisisha utolewaji wake bila kujikamua.
- Hakikisha unapata virutubisho kwa ajili ya kusawazisha bacteria wazuri ndani ya mfumo wa chakula, vyenye ubora wa hali ya juu usimeze kila kirutubisho.Kama huna chanzo kizuri cha kupata virutubisho hivi tunashauri fika ofsini kwetu kupata usaidizi.
Zingatia haya Ukiwa Chooni
- Ruhusu mwili wako kufanya kazi kwa jinsi ulivoumbiwa, yaani pale unapojiskia haja basi hakikisha unaenda mara moja kujisaidia pasipo kujizuia, kujichelewesha kunaweza kusababisha Constipation.
- Usikae mda mrefu chooni ukijisaidia, hii inaongeza mgandamizo katika eneo la chini kwenye mishipa ya damu na hivo kukuongeza hatari ya kupata bawasili. Tumia dakika 3 mpaka 5, ama subiri mpaka unapokuwa na haja, kama unajiskia kutoa uchafu lakni ukienda chooni kinyesi hakitoki basi tembea tembea ama fanya zoezi la Squats.
- Usitumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tumia misuli ya tumbo kutoa haja taratibu.
- Unapotoa haja basi hakikisha unachuchumaa kama miili yetu ilivoumbwa. Watu wanaotumia njia hii mara chache sana huugua bawasili, lakini matumizi ya vyoo vya kukaa ni moja ya kihatarishi cha kupata bawasili kutokana na kwamba inahitajika utumie nguvu kubwa sana kujikamua.
Tumi njia salama Kujisafisha
- Usitumie nguvu kubwa kujifuta kwa toilet paper ama wipes zingine baada ya kwenda haja, hii hufanya ngozi kulanika na kuvimba
- Kama inawezekana jisafishe taratibu kwa kutumia maji bila sabuni, na kujifuta kwa taulo laini.
- Kwa maeneo ambapo huwezi kutumia maji mfano kwenye vyoo vya umma, basi tumia wipes laini zenye unyevunyevu kwa umakini.
Fanya Yafuatayo Kupunguza Athari Ya Bawasiri Kama Tayari Umeugua.
Ushauri huu siyo kwamba hutakiwi kufika hospitali kupata huduma, ama kuonana na dactari wako . Ni ushauri ambao tunawapa wagonjwa wetu wote kabla hawajafika Ofsini kwetu kupata huduma ya Dawa na Virutubisho,
- Jaribu Sitz Bath, hii inajumuisha mgonjwa wa bawasili kuvua nguo na kukaa kwenye maji yenye uvuguvungu kwenye beseni kwa mda wa dak 15 mpaka 30, unaweza kukaa mara nyingi uwezavyo, hakiksha maji siyo ya moto ni ya vuguvugu, itakusaidia kupunguza maumivu.
- Chukua kipande cha barafu kilichoganda na kukiweka mahala pa haja kubwa kwa dak 10 mpaka 15 kwa siku.
- Chukua mmea wa Aloe-vera ukate kisha loweka kwenye maji, baada ya hapo chukua kitambaa laini loweka kwenye maji yenye aloe vera na upakae taratibu mahali pa haja kubwa.
MUHIMU,ushauri huu ni kwa ajili ya kupata nafuu ya haraka, hivo hakikisha unafika ofsini kwetu kupata huduma ya dawa na virutubisho, zingatia haya ili kutibu tatizo likaisha kabisa.
Madhara Ya Tatizo La Bawasiri
- kupata upungufu wa damu (anemia)
- Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo
- Upungufu wa nguvu za kiumekwa wanaume na Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
- kuathirika kisaikolojia
- kukosa moral ya kufanya Kazi na maumivu makali
Tiba ya bawasiri na ushauri kwa mgonjwa
Matibabu ya bawasiri yamegawanyika katika sehemu mbili na hutegemea na aina ya bawasiri
- Tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama ambayo hutoelewa hospital na kuendelea na lishe ya chakula. Hata hivyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia. Ndiomana katika kituo chetu tunashauri kutibu chanzo cha tatizo pasipo upasuaji.
- Tiba ya pili ya tatizo hili ni kwa kutumia vidonge vilivyotengenezwa kwa mimea.
Huduma hii ambayo inapatikana ofsini kwetu inajumuisha dawa na virutubisho kwa ajili ya kusafisha mfumo wa chakula,na hivo kuondoa uvimbe wowote ulio katika mfumo wa chakula.
Ikiwa na maana endapo kama kutakua na dalili za bawasili (uvimbe kwenye haja kubwa), pia hufanya kazi ya kurekebisha mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula na kumfanya mtu apate choo kwa ulaini na bila maumivu, kutibu vidonda vya tumbo na kuondoa tatizo la kiungulia ama acid reflux.
Tiba Asili ya bawasiri Tunayoweza kukupatia
Dawa hizi ni dawa asili zilizotengenezwa kwa mimea zenye nguvu (strength) ya 500 mg, zinakuwa kwenye mfumo wa vidonge/capsules na mafuta tiba.
Kumbuka.; Operation kwa kukata sehemu iliyoota inafeli mara nyingi kutibu tatizo hili kutokana na kwamba tatizo hujirudia tena na tena. Hivo tunashauri Tumia hizi dawa kwa muda wa siku 30, huku ukifata ushauri wa kitaalamu ambao tutakupa juu ya matumizi ya vyakula, tatizo litakuwa limekwisha.
Tiba yetu inajumuisha vidonge vya asili vya kumeza na mafuta ya kupaka ya black seed, dozi ya wiki mbili. Usihofu kuhusu gharama maana tunakupa huduma za uhakika kumaliza tatizo lako.
Kulingana na ukubwa wa tatizo lako tutapendekeza utumie dozi ngapi za dawa.
Gharama ya dawa ni Tsh 85,000/= ofisi zetu zipo Mwembechai , Magomeni.
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba :0678626254 kupata Huduma
Makala inayofuata: Chanzo cha muwasho mkunduni
²