Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na nini?

saratani ya shingo ya kizazi
kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi ni aina ya saratani ambayo hutokea kwenye eneo linalounganisha uke na mfuko wa mimba (uterus). Aina mbalimbali za virusi aina ya papilloma wamethibitishwa kusababisha saratani hii.

Mwanamke anapopata maambukizi ya HPV(human papilloma virus), kwa mara ya kwanza kinga yake hujaribu kupambana na virusi hawa ili wasilete madhara. Virusi hawa wasipodhibitiwa mapema  hupelekea  kuwepo ndani ya mwili kwa muda mrefu na wanaweza kuanza kushambulia seli za cervix (shingo ya kizazi) na kusababisha ukuaji wa seli za saratani katika eneo hili.

Mwanamke yeyote anaweza kupunguza hatari ya kupata saratani hii kwa kufanya vipimo mara kwa mara walau kila baada ya miezi mitatu au kupata chanzo dhidi ya maambukizi ya virusi wa papilloma.

Aina za saratani ya shingo ya kizazi.

Kuna aina mbili za seli kwenye kwenye shingo ya kizazi (cervix) ambazo ni squamous cell na glandular calls, hivo saratani ambayo huanzia kwenye seli za squamous huitwa squamous cell carcinoma na saratani inayoanzia kwenye seli za glandular huitwa adenocarcinoma.

Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba Saratani inapoanza huwa ni vigumu sana kuigundua kwani haioneshi dalili zozote. Hivo unaweza usigundue mpaka pale saratani imefikia hatua mbaya zaidi, pale ambapo dalili kama kutokwa na majimaji au maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Seli za kansa ya shingo ya kizazi  hukua taratibu na huchukua miaka michache kwa seli za kawaida kubadilika kuwa seli za kansa, ndio maana inashauriwa kufanya vipimo mara kwa mara ili kugundua na kuttibu mapema.

Dalili za Saratani ya Shingo ya Kizazi.

  1. Kutokwa na damu ukeni kusiko kawaida mfululizo
  2. Kupata maumivu makali ya tumbo na nyonga
  3. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  4. Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida.

Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.

Mgonjwa anapofika hospitali hufanyiwa kipimo cha Pap test. Kipimo hichi kinajumuisha kuchukuliwa kwa sample ndogo ya seli zilizoathirika kwenye cervix ili kugundua kama kuna mabadiliko na uwepo wa seli za saratani.

Watu gani wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya shingo ya kizazi zaidi?

Kuna sababu zilizo ndani ya uwezo wako ambazo unaweza kuzifanyia kazi na kupunguza hatari ya kupata saratani hii. Japo pia kuna njia ambazo ni vigumu kuepuka za ziko nje ya uwezo wetu kama vile uwepo wa saratani hii katika historia ya familia yako mfano kama mama ama dada yako aliwahi kupata saratani hii basi unaweza kuwa kwenye hatari kubwa nawe kupata. Makundi mengine ni kama

  • Wanawake kwenye umri kati ya miaka 20-50 wapo kwenye hatari Zaidi
  • Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
  • Kuzorota kwa kinga ya mwili husabisha kuongezeka kwa athari ya virusi wa HPV wanaoletekeza kansa ya shingo ya kizazi.
  • Wanaopata ujauzito katika umri mdogo chini ya miaka 17 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani hii.

Matibabu ya saratani ya Shingo ya kizazi

Tiba ya saratani ya shingo ya kizazi hutegemea na hatua ya ugonjwa husika, na inahusisha

  • Kufanyiwa upasuaji na kuondoa mfuko wa mimba (uterus) na viungo vingine kama ovari na mirija ya uzazi
  • Matibabu kwa kutumia dawa kali(chemotherapy) ili kuongeza muda wa kuishi
  • Matibabu kwa njia ya mionzi ili kuua seli za saratani.

HITIMISHO

  • Kwa kutegemeana na hatua ya saratani yako ilipofikia daktari anaweza kukuanzishia aina moja ya matibabu ama ukapata matibabu ya aina zaidi ya moja, hatua ya mwisho ni kuondoa kizazi kama saratani yako imesambaa sana. Kumbuka hatua hii itasababisha usiwe na uwezo wa kushika mimba tena. Jambo la kuzingatia kwa wewe mwanamke ni kufanya vipimo kila mara walau kila baada ya miezi mi3 ili kujihakikishia usalama wa afya. Pia hakikisha unatumia virutubisho mbalimbali kwa ajili ya kutoa sumu mwilini na kujikinga dhidi ya saratani.
  • Jaribu Cancer Care Package yetu: yenye virutubisho na dawa asili aina tatu zilizofanyiwa utafiti na kuhifadhiwa kwenye mfumo wa vidonge ambazo zitakusaidia
    1. Kuimarisha kinga ya mwili a hivo kuzuia kutokea kwa saratani
    2. Kupunguza madhara na dalili mbaya kama kutapika, maumivu, na uchovu kunakotokana na tiba ya Chemotherapy na Radiotherapy.
    3. Kusaidia kutibu saratani pale ambapo virutubisho hivi vitatumika pamoja na dawa za hospitali
    4. Kuzuia ukuaji wa seli za saratani na kusaidia uponaji haraka wa vidonda na
    5. Kuongeza uzalishaji wa seli nyeupe za damu kwenye mwili ambazo hupambana na seli za saratani.
      Unaweza kupata virutubisho hivi kwa kutembelea stoo yetu, bonyeza hapa. Au chati na daktari kwenye whatsapp kwa namba hapa chini.

Makala inayofuata,

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata Huduma

Share and Enjoy !

Shares
Shares