ABOUT

Karibu katika ukurasa wetu wa mtandaoni wa lindaafya.com.

Tunaamini kwamba binadamu wote tunapaswa kufurahia maisha pasipo kuumwa na kuteseka na magonjwa. Tumeumbiwa maisha yenye furaha na afya tele, swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza je tumefikaje hapa tulipo? Majibu yanaweza kuwa mengi lakini sababu kubwa ni lishe. Ndio ni lishe, lishe mbovu na uharibifu wa mazingia mazuri yanayotuzunguka imetufanya tuugue kila siku na kukosa furaha, ukianzia kwenye kemikali za kuua wadudu kwenye mimea, vyakula vilivyosindikwa, uchafuzi wa hewa na maji kutoka kwenye viwanda na tabia zingine hatarishi kama kutofanya mazoezi ni muunganiko wa hatari zinazopelekea tuumwe kila siku.

Sasa tujiulize tunaweza kuepuka moshi wa magari?, tunaweza kuepuka kula vyakula ambavyo vimelimwa bila kupigwa madawa?, tunaweza kuepuka kwa 100%, vyakula ambavyo havijapitia viwandani?, Jibu ni kwamba ni ngumu kuepuka kwa 100% hatari hizi zote maana ni sehemu ya maisha yetu kutokana na utandawazi na ugunduzi wa viwanda.

Tumaini letu lipo wapi?? Najua nawe pia unajiuliza tufanye nini sasa ili tuishi salama kama vihatarishi vyote hivi ni sehemu ya maisha yetu, tunafanya kazi viwandani, tunatumia maji yaliyotibiwa na kemikali, tunatumia vidonge, vipodozi na vyakula vyenye kemikali kwa wingi, muda mwingi tunautumia tukiwa tumekaa kwenye vitu, hatuna muda wa kufanya mazoezi sasa kwa mitindo hii ya maisha tunaweza kuepuka magonjwa kama kisukari, pumu, saratani, presha, upungufu wa nguvu za kiume, ugumba, kuvurugika kwa hedhi, na mengine mengi??

Habari njema ni kwamba bado kuna tumaini, ambalo litarudisha furaha na uwezo wa kuishi muda mrefu bila kuugua magonjwa ya lishe, magonjwa haya huwa napenda kuyaita magonjwa ya kisasa kutokana na kwamba yameshamiri sana kipindi hiki cha karne ya 21 baada ya ugunduzi wa viwanda. Tumaini letu ni kurudi zamani, ni kweli tunatakiwa kurudi na kutazama wapi tumekosea, babuzetu walikula nini na sisi tunakula nini, babu zetu waliishi vipi, walitumie dawa gani walipoumwa.

Hii ndio sababu yetu kuanzisha website hii, KURUDISHA FURAHA ILIYOKWEPO MWANZO YA KUISHI PASIPO KUUMWA., ambapo tunalenga katika kutatua changamoto za magonjwa sugu kwa kutoa ushauri na huduma ya dawa asili zisizo na kemikali hatari kwa mwili na virutubisho ambavyo vitajenga mwili na kukidhi mahitaji yako ya madini na vitamini muhimu, virutubisho kwa ajili ya kutoa sumu mwilini na kuzawazisha homoni zako.

Kuwa huru sasa kutuandikia muda wowote na kufika ofsini kwetu hapa Chinga Complex, floor ya 3, Karume Dar es salaam.

Email. info@lindaafya.com

Share and Enjoy !

Shares
Shares