Genital Warts Husababishwa Na Nini
Genital warts ni hali ya kuota vinyama sehemu za siri ambako husababishwa na virusi wa HPV(Human Papiloma Virus). Virusi hawa waligunduliwa na mwanasayansi mjerumani aitwae Harold zur Hausen alipokuwa akifanya utafiti.
Katika utafiti wake bwana Zur Husen aligundua kua wanawake wenye genital warts walianza kupata saratani ya shingo ya kizazi(cervical cancer). Ripoti ya shika la afya duniani zinasema kwamba kuna aina Zaidi ya 100 ya virusi wa papilloma waliokwisha kugunduliwa mpaka sasa ambapo kati ya hao ni aina mbili tu HPV-6 na HPV-11 husababisha genital warts.
Genital Warts/Vigwaru Huonekanaje?
Genital warts huonekana kama vinyama vidogodogo vya rangi ya kijivu na nyekundu vinavyoota mahali popote kwenye mwili, kwenye uume au uke. Zinaweza kuota kama kinyama kimoja moja au kufanya mkusanyiko mahali pamoja. Vinyama hivi vinaweza kuota pia kwenye mapaja na sehemu ya haja kubwa
Imani Potofu Kuhusu Ugonjwa Wa Genital Warts
Genital warts zinaweza kusababisha saratani ya shingo kizazi:
Ni kweli kwamba maradhi yote haya husababishwa na virusi wa HPV. Lakini pale maambukizi yanapokuwa madogo basi warts au misundosundo/vinyama huota sehemu mbalimbali za mwili. Kadiri athari ya virusi inavoongezeka bila kutibiwa mapema kwa mwanamke basi hupelekea kupata saratani ya shingo wa kizazi.
Virusi vya HPV (human papilloma virus) vinatibika
Ukweli ni kwamba virusi hivi huwa havitibiki mpaka sasa hakuna dawa, ila kinachofanyika ili kumsaidia mgonjwa ni kutibu dalili za tatizo husika na kuongeza kinga mwili uweze kupambana wenyewe na virusi hawa.
Wanawake pekee huambukizwa virusi wa HPV
Tafiti zinaonesha Wanaume wanaofanya ngono zaidi na zisizo salama huweza kuambukizwa virusi hawa pia. Watoto pia huambukizwa virusi hawa pale wanapoathirika na au kupata mguso wa virusi wa papilloma kwenye ngozi zao.
Wanawake wanaofanya ngono za jinsia moja hawapati maambukizi ya HPV
Virusi wa HPV huambukizwa pale ngozi iliyoathirika inapogusana na ngozi yenye afya. Hivo makundi yote ya watu wapo kwenye hatari ya kupata maambukizi endapo wakiambatana na watu walioathrika.
Inakuwaje Mpaka Mtu Anapata Genital Warts.
Virusi wa papilloma kwa kiasi kikubwa husambazwa kwa njia ya ngono. Ikijumuisha kufanya ngono kupitia mdomo na njia ya haja kubwa na njia ya kawaida).
Ni muhimu mpenzi msomaji wa makala hizi ukumbuke kwamba kuna aina nyingi za virusi wa papilloma lakini wanaosababisha genital warts ni aina mbili ambazo ni (HPV-6 na HPV-11).
Ili kugundua kama tayari una genital warts, daktari hufanya uchunguzi wa kawaida kwa kutumia macho na kuangalia dalili za tatizo husika. Baada ya hapo ili kujiridhisha anaweza kukata kiasi kidogo cha tissue kutoka kwenye warts kufanyiwa vipimo maabara.
Tabia Hatarishi Zinazoweza Kukupelekea Kupata Genital Warts.
- Kufanya ngono isiyo salama na mtu aliyeathirika na HPV: Ni muhimu kutumia kinga kama condoms ili kuzuia maambukizi, hii ni muhimu sana kwa wale wenye wapenzi wengi au wanaojihusisha na ngono kupita kiasi.
- Oral sex, au ngono kupitia mdomo: kufanya ngono kwa kutumia mdomo inakuweka katika hatari ya kupata warts au kuota vinyama sehemu za mdomo.
- Ngono katika umri mdogo: Watu wanaoanza ngono mapema wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata genital warts kutokana na kinga za mwili kua chini sana.
Matibabu Ya Genital Warts
Tiba ya tatizo hili hupatikana kirahisi iwapo tatizo halijachelewa kupatiwa tiba. Matibabu hutolewa kwa kufuata utaratibu wa majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali. Matibabu hayo huweza kuwa ya kuviondoa vinyama kwa kufanya operations au kutumia dawa.
Hata hivyo njia ya operation sio nzuri sana kwasababu huweza kutengeneza madhara zaidi na uwezekano mkubwa wa tatizo kujirudia. Tiba nzuri ni kutumia dawa ambazo zitatibu na kuondoa tatizo hilo na mgonjwa kupona kabisa.
Cha kuzingatia ni kwamba ugonjwa huu ni wa kuambikiza hivyo inashauriwa wenza wote kupata matibabu hata kama atajihisi hana dalili yoyote ni vyema akafanya vipimo ili kujihadhari kabla ugonjwa haujaleta madhara Zaidi.
Kwa Upande wa tiba zetu asili tutakupa vidonge asili vya Propolis ili kutibu tatizo hili ndani ya wiki mbili. Dawa ipo kwenye mfumo wa vidonge, unameza kila siku kwa wiki mbili tu.
Tembelea ofisi zetu za Dar es salaam, kupata elimu, ushauri na huduma ya dawa.