Kushindwa kuzuia mkojo wakati wa tendo la ndoa ni kesi inayowatokea watu wengi. Kwa kiasi kikubwa hutokea zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.
Asilimia 60 ya wanawake wanaoshindwa kuzuia mkojo hupata tatizo hili la kukojoa wakati wa tendo. Hapa kuna tofauti kidogo kati ya kujoa kwa maana ya kutoa majimaji baada ya kufika kileleni, na kukojoa mkojo wa kawaida.
Kufika kileleni
Watafiti wanasema kwamba baadhi ya wanawake wanapofika kileleni baada ya msisimuko wa hali ya juu, hutokwa na maji ya rangi nyeupe ambayo huzalishwa na tezi zilizopo kwenye kuta za uke. Maji haya hufanya kazi ya kulainisha uke na pia kusafisha njia ya uke kwa ajili ya mbegu za kiume kupita vizuri.
Kikawaida pale unapofanya ngono hii ni kwa wote mwanaume na mwanamume, njia ya mkojo huziba na kubaki njia ya uzazi.
Nini kinasababisha Kushindwa Kuzuia Mkojo wakati wa tendo la ndoa.
Kukojoa wakati wa tendo la ndoa mara nyingi hutokana na kushindwa kujizuia (incontinence). Yaani mkojo kutoka pasipo matarajio. Zifuatazo ni sababu zinazopelekea ushindwe kujizuia na kuachia mkojo wakati wa tendo la ndoa.
Kutokwa na Mkojo pasipo hiari (Urinary incontinence)
Wanawake wanaweza kuvuja mkojo pasipo hiari wakati wa tendo la ndoa na pale wakifika kileleni. Msisimuko wa tendo la ndoa unaweza kuongeza mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo. Mgandamizo huu ukiambatana na kusinyaa kwa misuli ya nyonga inaweza kusababisha mwanamke kutokwa na mkojo pasipo hiari.
Sababu hatarishi Zinazokupelekea Ushindwe kujizuia Mkojo.
Baadhi ya watu wanaweza kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kushindwa kujizuia mkojo kutokana na sababu zifuatazo
- Kuwa mjamzito au kutoka kujifungua
- Wanawake walikoma hedhi wako kwenye hatari zaidi
- Kwa wanaume kukua kwa tezi dume ama upasuaji wa tezi dume
- Mawe kwenye kibofu cha mkojo
- Uzito mkubwa na kitambi
- Maambukizi kwenye njia ya mkojo, tezi dume na kwenye kibofu
- Kuathirika kwa neva kutokana na kisukari au stroke
- Matumizi ya dawa mfano za presha na msongo wa mawazo
- Matumizi ya pombe
- Magonjwa ya akili na
- upasuaji kwenye njia ya mkojo na na njia ya uzazi
Jinsi ya Kugundua na Kutibu Tatizo
Kama unafahamu kwamba unatoa mkojo wakati wa tendo la ndoa, ongea na daktari wako. Daktari anaweza kukufahamisha kama ni mkojo ama ni majimaji tu baada ya kufika kileleni. Kama ni mkojo daktari atakwanzishia huduma ya tiba kwa tatizo lako ili kuimarisha uwezo wa kujizuia mkojo kutoka bila hiari.
Hatua ya kwanza: Kuimarisha Misuli ya nyonga
Kama ni mwanamke daktari anaweza kupendekeza kufanya baadhi ya mazoezi ya misuli ikiwemo kegels.
Kegel exercise huongeza uimara kwenye misuli ya nyonga ambayo inashikilia viuongo vya uzazi. Mazoezi haya pia husaidia kuimarisha misuli ya njia ya mkojo (sphincter muscles) ili kuzuia mkojo kutoka bila hiari. Mazoezi ya kegel husaidia pia
- Kuimarisha uwezo wa kibofu kuhimili mkojo
- Kuimarisha uwezo wa kuhimili haja kubwa na
- Kuongeza mzunguko wa damu kuelekea kwenye via vya uzazi na hivyo kuongeza raha ya tendo ndoa (sexual pleasure)
Kwa wanaume mazoezi ya kegel yanasaidia kuimarisha uwezo wa kudhibiti mkojo na pia kuimarisha kusimama kwa uume wakati wa tendo la ndoa.
Tafiti zinasema kwamba wanaume wanaofanya kegel kwa miezi 6 tatizo la kutosimama kwa uume huisha kabisa.
Mazoezi haya unaweza kufanya muda wowote ukiwa umekaa, umesimama, au umelala na yanaweza kufanywa kila sehemu. Ni viuri kwa kutoa mkojo wote kabla hujaanza zoezi hili.
Jinsi ya utambua Misuli ya kuimarisha.
Misuli hii utaitambua pale unapokojoa, kisha bana mkojo usitoke. Misuli unayotumia kusimamisha mkojo usiendelee kutoka ndio utakayoifanyia kazi.
Baada ya kutambua misuli hii, anza kubana ukiwa popote pale kwa sekunde tano na kuachia ukiwa huna mkojo. Hakikisha usikaze matako au tumbo au miguu . Rudia mara 20 kwa mara moja na kisha fanya tendo hili mara tatu kwa siku.
Hatua ya 2. Mazoezi ya Kibofu.
Mazoezi ya kibofu yatakusaidia kwenda mda mrefu zaidi kabla ya kukojoa. Mazoezi haya yanaweza kufanyika kwa kushirikisha na yale ya kegel. Kuzoesha kibofu chako hakikisha unajiongezea muda kutoka ulipokojoa mara ya mwisho na pale unapopata mkojo mara nyingine.
Ongeza taratibu mfano dakika 15 mpaka kufikia masaa maatatu au ma4. Kumbuka no zoezi la taratibu na linaweza kuchukua week 6 mpaka 12 kwa mwili kuzoea.
Hatua ya 3. Badili Mtindo wa Maisha
- Jaribu staili tofauti tofauti za kufanya mapenzi. Hii itakusaidia kugundua staili inayokupa furaha zaidi.
- Hakikisha unatoa mkojo kabla ya kuanza tendo la ndoa
- Kama unna uzito mkubwa na kitambi anza programu ya kupunguza unene sasa. Unaweza kupata kutumia virutubisho vyetu kwenye stoo.
- Jizuie matumizi na ya vinywaji vyenye pombe na caffeine ambavyo huongeza haja ya kukojoa
- Epuka kunywa vimiminika wakati unakaribia kuanza tendo la ndoa. Hii itapunguza kiasi cha mkojo kwenye kibofu.
Maelezo ya mwisho.
Kwa watu wengi tatizo la kupata mkojo wakati wa tendo huisha baada ya muda flani, kwa kubadilisha tu mtindo wa maisha na kufanya mazoezi. Kwa watu wegine tatizo linaweza kuendelea. Ni vizuri kuonana na Daktari kama utajaribu njia zote hizi pasipo mafanikio.