Saratani ya damu-Leukemia

saratani ya damu

Leukemia ni  nini

Leukemia ni saratani ya damu, yaani inaathiri seli za damu. Ukirejea somo la sayansi darasa la tano tulijifunza kwamba damu imetengenezwa kwa seli aina tatu ambazo ni: Platelets husaidia damu kuganda, seli hai nyekundu (RBCs) zinazohusika na kusafirisha hewa safi ya Oxygen mwilini, seli hai nyeupe (WBCs) ambazo hutoa kinga dhidi ya maambukizi ya bacteria, fangasi, virusi na wavamizi wengine wa mwili.

Saratani ya damu huathiri seli nyeupe za damu. Seli nyeupe za mgonjwa wa Leukemia zinakuwa siyo za kawaida (abnormal) na hazifanyi kazi yake inavotakiwa. Seli nyeupe za damu hutengenezwa kwenye uboho (bone marrow) na bandama.

Dalili hizi Zinaonesha Kwamba Tayari una Saratani ya Damu (Leukemia)

  • Kupata jasho jingi kupita kiasi hasa wakati wa usiku (night sweets)
  • Mwili kukosa nguvu na uhitaji wa kupumzika mara kwa mara
  • Kupungua uzito kwa kasi
  • Maumivu ya mifupa na mifupa kuwa laini
  • Kupata vimbe ambazo haziumi (lymph nodes) hasa kwenye kwapa na shingoni
  • Kutanuka kwa ini na bandama
  • Ngozi kupata vipele kwa haraka na kutoa damu kiurahisi, mfano kila unapojikuna ngozi inawahi kutoa damu
  • Kupata homa
  • Maambukizi ya mara kwa mara na
  • Kuvuja kwa damu kutokana na kupungua kwa uwezo wa damu kuganda

Dalili zingine za Leukemia huwa zinategemea na athari ya saratani kwenye kiungo husika. Mfano ma athari imetokea kwenye mfumo wa kati wa neva basi mgonjwa atapata dalili kama maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutapika, kushindwa kwa misuli na mwili kukakamaa. Saratani ya damu inaweza kusambaa na kuathiri viungo vingine kama mapafu, moyo, korodani na figo.

Mazingira Hatarishi Yanayoongeza Uwezekano wa Kupata Saratani ya Damu.

  • Historia ya familia:k Kama mmoja wa mtu kwenye familia aliwahi kuugua saratani ya damu basi ndugu wengine wanaweza pia kuugua
  • Uvutaji wa sigara
  • Watu wenye magonjwa ya damu
  • Watu waliowahi kupata matibabu ya saratani kama radiotherapy na chemotherapy
  • Wanaofanya kazi sehemu za mionzi

Tiba Kwa Leukemia

Tiba ya Saratani ya damu (Leukemia) hutegemea na aina na stage ya saratani ilipofikia. Baadhi ya aina za Leukemia hukua taratibu na hazihitaji tiba ya haraka. Tiba ya saratani ya damu inajumuisha

Chemotherapy: ambapo dawa hutumika kuua seli za saratani. Kutokana na aina ya saratani yako dactari anaweza kushauri upewe dawa aina moja ama muunganiko wa dawa.

Tiba ya mionzi (Radiotherapy), mionzi mikali hutumika kuua na kuzuia ukuaji wa seli za saratani. Mionzi inaweza kupigwa mwil mzima ama kwenye eneo fulani.

Kupandikizwa kwa seli mpya (stem cell transplantation) : seli hizi hupandikizwa kwenye eneo la ndani ya mfupa ambapo seli nyeupe huzalishwa.

Immune therapy: ambapo ni tiba inayolenga kuimarisha kinga ya mwili ili kuzuia kusambaa kwa seli za saratani.

Jinsi Saratani ya damu (Leukemia) Inavotokea

Saratani ya damu (Leukemia) inaaaminika kutokea baada mabadiliko kwenye vinasaba. Mabadiliko ambayo hupelekea kutengenezwa kwa seli zisizo za kawaida. Seli hizi huongezeka katika kipindi fulani na kuwa nyingi kuliko seli nzima. Hapo ndipo dalili mbaya za leukemia huanza kujitokeza.

Ni Muda Gani Unapaswa Kumwona DaKtari

Pale unapoona dalili za muda mrefu ambazo siyo za kawaida basi weka apointimenti ya kuonana na daktari ili kufanya vipimo na ushauri. Mara nyingi dalili za Leukemia huwa haziko wazi na zinafanana na dalili za matatizo mengine ya kiafya. Ndio maana kuna umuhimu wa kufika hospitali kila unapoona dalili za hatari.

Dawa na Tiba zetu Asili

Lengo la dawa na tiba yetu siyo kukatisha tiba ya hospital. Lengo letu ni kukusaidia upate nafuu mapema wakati unaendelea na tiba ya hospital. Pia dawa zetu asili

  • zinapunguza makali ya saratani
  • kuimarisha inga ya mwili
  • kupunguza kasi ya kusambaa kwa saratani
  • kuondoa dalili mbaya kama maumivu ya mifupa na uchovu na
  • kupungiuza athari ya mionzi kwa mgonjwa aliyeanza tiba ya hospital

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata huduma ya virutubishi kwa mgonjwa , Kwa gharama ya Tsh 250,000/=

Share and Enjoy !

Shares
Shares